Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi ambao makazi yao yalikuwa yamebomolewa.
Jumla ya nyumba sitini na nane (68 )zenye wakazi zaidi
ya 100 katika Mtaa na kata ya Bombambili Wilaya na Mkoa wa Geita zimebomolewa
kwa madai kuwa wananchi waliokuwa wakiishi kwenye makazi hayo wamevamia hifadhi
ya Mistu bila ya ridhaa ya wakala wa mistune nchini(TFS) huku kukiwa na
malalamiko kwa baadhi ya wananchi wenye uwezo wakiachwa katika Eneo hilo bira
kuvunjiwa.
Maduka online imefika katika Eneo hilo majira ya saa
nane Mchana na kushudia tinga tinga likiendelea na ubomoaji huku wanachi
wakiendelea kutoa baadhi ya thamani nje ya nyumba hizo huku jeshi la
polisi likiwa na Mabomo ya machozi
pamoja na Risasi za moto kwa lengo la kuimalisha ulinzi wakati wa zaoezi hilo.
Wakizungumza na Maduka online wananchi hao walisema kuwa pamoja na Serikali
kuwabomolea kwa kukaa hapo kimakosa hata hivyo mshangao unakuja kutokana na
kwamba wanaobomolewa ni wao wenye hali ya chini wale wenye uwezo nyumba zao
zimeachwa hali ambayo imepelekea kumwomba Rais John Magufuli kuwasaidia walau
makazi ya kuishi kutokana na ugumu wa maisha ndio chanzo cha wao kuvamia maeneo
ya hifadhi ya Mistu.
“Tuliishi kwa miaka mingi sana na viwanja tuliuziwa na
viongozi wa mitaa kwa barua na tulianza ujenzi mara moja lakini leo wamekuja na
kuanza kubomoa kwa madai tumevamia Hifadhi ila kinachosikitisha kuna Nyumba za
vigogo zimebaki kwenye Eneo wanalosema ni Mstu hapa kuna uonevu Mkubwaa sana
Tunaomba Rais asikie Kilio chetu”alisema Aginesi John Mkazi wa mtaa huo.
“Mimi ni mjane nilipoteza mme wangu tangu mwaka 2011
aliniachia watoto 5 nasomesha mimi ndiye baba Nyumba yangu wamebomoa na vitu
vyangu viko nje kama mnavyoona nitakwenda wapi nitalala wapi, nitakula wapi, mi
sina ndugu hapa Geita na wakati wansema Serikali ya Rais John Pombe Maguli ni
ya wanyonge lakini sisi tunazidi kukandamizwa kama mlivyoshudia alisika akipiga
Mayoe”Gaudesia Mathias.
Meneja wa TFS Wilaya ya Geita Fredy Ndandika alisema opalesheni hiyo
ilianza tangu mwaka jana na wanachi walikuwa na taarifa za kuondoka na kupisha
hifadhi huku akikanusha taarifa za kwamba walivamiwa na kuanza kubomoa na
kuwata kuanza kufata sheria zilizowekwa na Mistu kwa kuzieshimu.
“Tulikuja hapa tangu Mwaka jana na kuanza kutoa
matangazo kwa wananchi waliovamia Msitu wa Geita lakini waligoma kuondoka ndio
maana leo tumeamua kuvunja kwa kutumia nguvu na tataendelea kuwaondoa na
kuvunja Nyumba zote za watu waliovamia Hifadhi za Mistu”alisema Ndandika .
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na
usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alikuwa
msimamizi wa zoaezi hilo alisema kuwa wakati maeneo hayo yanatolewa yeye akuwa
kiongozi Ndani ya Wilaya hiyo laki amesema kama wananchi waliuziwa maeneo hayo
kwa kudanganywa wapeleke vielelezo Ofisini kwake kuanzia siku ya jumatatu na
waliousika watachukuliwa hatua kali kwa kuwadanganya wenzao.
“Mimi nafata maagizo yaliotolewa na Naibu Waziri wa
Mazingira lakini kama kuna wananchi wangu waliuziwa viwanja na Viongozi kwa
kudanganywa wavilete siku ya jumatatu Ofisini kwangu nitasimamia watarudishiwa
fedha zao na kuchukuliwa hatua kali kwa kuwaibia wenzao kwani huo ni wizi kama
wizi mwingine”alisema Kapufi.
Hivi Karibuni wakati wa Ziara yake
Mkoani Geita Naibu Waziri wa Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi hao
ambapo aliwaomba kuondoka kwa hiyari kwenye hifadhi hiyo na kwamba wafate
taratibu ambazo zimewekwa na serikali .
Imeandaliwa na Maduka Online
|
Post A Comment: