Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (aliyekaa kulia) na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Na Lawrence
Raphaely-Bunge.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Job Ndugai amewaahidi Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania
ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama hicho ikiwemo
maadhimisho ya Siku ya Skauti Afrika na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti
hapa nchini.
Mhe Spika
aliyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Skauti
Tanzania Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
ambao walimuomba awaunge mkono katika shughuli zao.
Spika Ndugai
aliwaeleza Viongozi hao kwamba kwa niaba ya Wabunge wote ameupokea ujumbe huo
na atajitahidi sana katika kuhufikisha kwa Waheshimiwa Wabunge.
“Ninawashukuru
sana kwa ujumbe huu na niwaahidi kwamba tupo pamoja si katika hili tu bali
katika mambo yoyote ambayo mtakuwa mkiyafanya na nawaahidi pia ushiriki wa
Waheshimiwa Wabunge katika maadhimkisho hayo,” alisema Mhe Spika.
Awali
akimuelezea Mhe Spika kuhusiana na Shughuli mbalimbali za Skauti hapa nchini
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Stella Manyanya ambaye
aliambatana na Viongozi hao wa Skauti alisema pamoja na majukumu mengine Chama
hicho cha Skauti kina kazi kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Skauti Dunia
na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.
Mhe Manyanya
alisema kuwa maandalizi ya Maadhimisho ya siku Skauti Afrika ambayo
yanatarajiwa kufanyika tarehe 8 hadi 11 Machi mwaka huu mkoani Arusha
yanaendelea vizuri ingawa kuna changamoto kubwa ya kifedha katika maandalizi ya
maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini ambayo yanatarajiwa
kufanyika kuanzia Juni hadi Julai Mkoani Dodoma.
“Mhe Spika
kumekuwa na jitihada mbalimbali za kufanikisha maadhimisho haya lakini kumekuwa
na changamoto katika kufikia malengo na ndio maana tumefikana hapa ili kukuomba
utuunge mkono” alisema Mhe Manyanya.
Mhe Manyanya
aliongeza kuwa Wizara imendelea kutambaua kazi kubwa ambayo Chama cha Skauti
inafanya katika kuendelea kuhimiza nidhamu miongoni mwa Vijana na kuwajengea
moyo wa kujitolea.
“Chama hiki
Mhe Spika kimekuwa kikiendelea kufanya kazi kubwa katika kuwajengea Vijana wetu
moyo wa kujitolea na kwa sasa tunataka kazi zao zifanyike kwa nguvu zaidi
tofauti na hapo mwanzo”
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya
Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga alisema anathamini sana mchango wa Mhe
Spika na kwamba anashukuru kwa kauli yake ya kuwaunga mkono.
Balozi
Kuhanga aliongeza kuwa kwa sasa Uongozi wake unajipanga katika kuhakikisha kuwa
Skauti inazidi kukua hapa nchini.
“Mhe Spika
nia ni kuona Vijana wa Shule za Msingi hadi Chuo Kikuu wanaingia katika Skauti
na hivyo tunataka twende mbele zaidi ya hapa tulipo kwa sasa,” alisema Balozi
Kuhanga.
|
Post A Comment: