Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa BAVICHA
Mkoani Geita,Neema Chozaire wakati wa kikao cha mpango kazi kilichofanyika
mjini Geita.
Bi,Chozaire
alisema kuwa kitendo hicho ambacho kimefanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
ni uzalilishaji mkubwa kwa kiongozi wao kwani hakuna ushahidi ambao unamwonesha
kuwa ni mtumiaji na muuzaji wa madawa ya kulevya hivyo kitendo cha kumtangaza
hadharani kiongozi wao ni ukiukwaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
“Tunawaomba
watanzania wapuuze vikali kwani hii ni siasa inachezwa na kuna kauli zilishawai
kutokea kwamba watahakikisha wanauwa vyama pinzani na ndio maana RC Makonda
hakuona hatari kuwataja viongozi kuwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya kweli
imetuuma sana na pia tumesikitishwa sana na kitendo hiki ambacho kimefanywa na
Makonda”Alisema Chozaire.
Mwenyekiti
wa Bavicha Jimbo la Geita Mjini,Deogratias Shinyanga,alielezea kuwa kesi ambayo
ipo mahakamani sio ya kwamba amepandishwa
kwa sababu anajihusisha na madawa ya kulevya kwani kiongozi wao ameenda kuomba tafsiri ya kikatiba juu ya mamlaka ambayo anayo mkuu wa mkoa kuitisha watu na kumtangaza kiongozi huyo.
Aidha kwa
upande wake Katibu wa Bavicha Wilaya ya Geita Nguru Bright,alisema kuwa kitendo cha kutangazwa kwa mtuhumiwa
kabla ya kukamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani ni sawa na kuingilia
mamlaka ya jeshi la polisi na mahakama kwani kumtangaza mtu kesi ingekuwa
imesomwa na kubainishwa kama ni kweli
mtuhumiwa anahusika na madawa ya kulevya.
Hatua ya
BAVICHA imekuja mara baada ya kiongozi na mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya
Taifa kuhusishwa na matumizi pamoja na
uuzaji wa madawa ya kulevya.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Post A Comment: