Wajumbe wakikao wakifatilia.
Wananchi
Mkoani Geita,wametakiwa kutoa ushirikiano wa karibu kwa watafiti wa viashiria na matokeo ya ukimwi kwa mwaka 2016
ambao watafika kwenye maeneo 12 ambayo
yamepangwa kufanyiwa utafiti.
Wito huo
umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati
wa Mkutano wa wadau wa utafiti wa
viashiria na matokeo ya ukimwa ya mwaka 2016 uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa
alisema kiwango cha maambukizi kuwa
kwasasa maambukizi yamepungua kwa asilimia mbili hali ambayo imesaidia
kuhifanya Tanzania kuonekana kuwa chini katika ukanda wa jangwa la sahara.
“Kiwango cha
maambukizo ya VVU katika tafiti zilizopita kinaonekana kupungua kutoka asilimia
7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011. Taarifa hii inaonyesha kuwa juhudi
hizo za Serikali zimeiwezesha Tanzania kupunguza kiwango cha maambukizo ya VVU
kwa asilimia mbili na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango
cha chini cha maambukizo kati ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ambapo
nchini nyingi za ukanda huu zina kiwango cha maambukizo cha zaidi ya asilimia
10”Alisema Kyunga
Kwa upande
wake afisa mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba ameelezea
kuwa katika mikoa ambayo wamepita wamepata ushirikiano wa mwitiko mkubwa kutoka
kwa wananchi ambao walikuwa wakiwafikia kwaajili ya shughuli ya upimaji.
“Kiukweli
mikoa ambayo tumepita kwaajili ya zoezi hili tumepata ushirikiano mkubwa sana
changamoto hazikosekani tulikutana na changamoto baadhi ya watu ambao walikuwa wameandikishwa
kukosekana kwenye makazi yao kwa maana ya kwamba wameama makazi"Alisema Bupamba.
Pamoja na hayo
utafiti huo utasaidia kukusanya taarifa za upatikanaji na utumiaji wa huduma zitolewazo katika
kudhibiti maambukizo ya VVU na Ukimwi na
vile vya tabia hatarishi vinavyochangia maambukizo ya VVU.
Utafiti wa
namna hiyo ni wa awamu ya nne kufanyika nchini ,unaoangalia zaidi maswala ya
afya ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004,wa pili ulifanyika
2007/2008 na utafiti wa tatu ulifanyika 2011/2012
IMEANDALIWA NA MADAKA ONLINE.
|
Post A Comment: