Mbunge wa
Geita Mjini Constatine Kanyasu amesikitishwa kwa kitendo cha wananchi waliokuwa
wamejenga kwenye hifadhi ya misitu kubomolewa huku wengine wakiachwa katika
maeneo hayo na kuahidi kushughulikia ili haki itendeke sawa na wale ambao hawajabomolewa.
Hayo
aliyasema kwenye mkutano wa hadhara
ambao umefanyika kwenye mtaa wa Mwatulole kata ya buhala hala wilaya na Mkoa wa
Geita,wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika jimbo ambalo
analiongoza.
Mh Kanyasu
amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya TFS kubomoa nyumba za watu wengine huku
wale wenye uwezo wakiachwa na kuendelea kukaa kwenye maeneo hayo kutokana na
hilo wameagiza watu wa TFS kuangalia kama wale waliobomolewa pale yalikuwa ni maeneo yao na ninani ambaye aliwauzia.
“Naomba
Nikiri na mimi iliniuma sana lakini kwa sababu ni serikali na sikuwepo na sijui kama walitumia sheria
mimi naomba yeyote ambaye ni haki yake ya msingi alete na mimi nitashughulikia”Alisema
Kanyasu
Hata hivyo
Bi,Chausiku Lusetula ambaye ni miongoni mwa wanananchi waliobomolewa makazi yao
amemuomba Mbunge kuwasaidia ili wapate haki zao za msingi na kwamba kwa sasa
hawana makazi ya kuishi baada ya makazi yao kubomolewa.
“Mheshimiwa
Mbunge sisi ni watu ambao tumekosa makazi kwa sasa hatujui ni wapi tutaishi na
chakusikitisha kwanini sisi tubomolewe na wengine waendelee kukaa kwenye maeneo
ambayo inasemekana ni hifadhi ya misitu kama ni hivyo ni vyema haki itendeke
kwa wote”Alisema Chausiku
Diwani wa
kata ya Buhala hala ,Mussa Kabese amewaambia wananchi kuwa mbunge wa jimbo la
Geita Mjini tayari amekwisha mwandikia Waziri mwenye dhamana barua ambayo
imemwomba matumizi ya pori la buhala hala kubadilishwa na kuwekwa taasisi ambazo zitawasaidia
wananchi ambao wapo kwenye mitaa ya shinde na magogo kupata mahitaji ya msingi ikiwemo swala la elimu na afya.
Hatua hii
imekuja ni baada ya takribani wiki mbili kumalizika ambapo wananchi ambao
wamejenga kwenye hifadhi ya misitu inayosimamiwa na wakala wa misitu nchini TFS kubomolewa makazi yao.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: