WADAU WA ELIMU KUTOKA UINGEREZA WAITEMBELEA MANISPAA YA ILEMELA NA KUFURAHISHWA NA MIKAKATI YAKE.

Share it:


Mkuu wa shule ya Saekondari Ibinza, Mwl.Igweselo Kahayi (kulia), akisalimiana na Judith Martin kutoka taasisi ya Wabia Network.
Mkuu wa shule ya Saekondari Ibinza Mwl.Igweselo Kahayi, akiwatambulisha wageni hao mbele ya wanafunzi wa shule hiyo (hawapo pichani).
Mbunge wa jimbo la Ilemela, Dkt.Angeline Mabula, akizungumzu na wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinza ambapo alisema juhudi zinafanyika ili kila mwanafunzi aweze kuwa na kitabu chake kutoka hivi sasa ambapo kitabu kimoja hutumika na wanafunzi watatu huku akiahidi kutoa zawadi kwa wanafunzi na waalimu watakaokuwa wakifanya vyema kwenye mitihani yao ya kitaifa.
Katibu wa ofisi ya mbunge jimbo la Ilemela, Heri James, akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinza walipotembelewa na wadau wa elimu kutoka taasisi ya Wadia Network ya nchini Uingereza
Mdau wa elimu, Judith Martin (kushoto) kutoka taasisi ya Wabia Network ya nchini Uingereza akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinza na kufurahishwa na maendeleo ya shule hiyo baada ya taasisi yake kusaidia upatikanaji wa vitabu vya sayansi na kuahidi taasisi hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wake katika kuinua kiwango cha elimu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinza, wakimsikiliza Judith Martin kutoka taasisi ya Wabia Network ya nchini Uingereza.
Diwani wa Kata ya Nyamuhongolo, Andrew Nginila, akitoa salamu za shukurani kwa wadau wa elimu kutoka Wabia Network na kuhimiza ushirikiano zaidi katika kutatua baadhi ya changamoto za kielimu katika kata hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Ibinza akitoa shukurani kwa wadau wa elimu kutoka taasisi ya Wabia Network ya nchini Uingereza ambapo alihimiza wadau zaidi kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto za kielimu ikiwemo utatuzi wa vitendea kazi.
Picha ya pamoja baina ya wanafunzi wa Ibinza Sekondari na wadau wa elimu kutoka taasisi ya Wabia Network ya nchini Uingereza pamoja na wenyeji wao, ofisi ya taasisi ya The Angeline Foundation iliyochini ya mbunge wa Ilemela Dkt.Angelina Mabula.



Mkuu wa shule ya Saekondari Ibinza iliyopo Kata ya Nyamuhongolo katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Mwl.Igweselo Kahayi (kulia), jana akikabidhi taarifa yake kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Wabia Network ya nchini Uingereza, Steve Martin (kushoto).

Ni baada ya shule hiyo kuwa miongoni mwa shule zilizonufaika na vitabu vya sayansi vilivyotolewa na taasisi hiyo kupitia taasisi ya mbunge wa jimbo la Ilemela, Dkt.Angelina Mabula ambayo ni The Angeline Foundation.

Mwaka 2015 taasisi ya Wabia Network ilitoa takribani shilingi Milioni Nane ambazo zilitumika kununulia vitabu 600 vya sayansi ambayo vilipelekwa kwenye shule za Ibinza, Kilimani na Mihama ambazo zilizofanya vibaya katika matoke ya kitaifa mwaka huo.

Mbunge wa jimbo la Ilemela, Dkt.Angeline Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alibainisha kwamba baada ya shule hizo kupokea vitabu hivyo, zimeweza kubadili matokeo yake na kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya mwaka jana ambapo wilaya ya Ilemela ilikuwa miongoni mwa wilaya 10 bora zilizofanya vizuri kielimu.
#BMGHabari



Share it:

habari

Post A Comment: