Huduma ya maji katika mji wa
Geita Bado ni tatizo kubwa kwani watu ambao wanapata maji safi na
salama kwa sasa ni Asilimi 36 huku lengo
la serikali ni kuhakikisha asilimia 90 wanapatiwa huduma ya maji katika miji.
Akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara ambao umefanyika katika kata ya Nyankumbu mmoja kati ya wananchi, Bi,Angelina
Richard amemwambia mbunge wa Geita Mjini ,Constatine Kanyasu kuwa tatizo
la maji limekuwa ni tatizo kubwa hususani kwa wakina mama hali ambayo imekuwa
ikitishia kuvunjika kwa miji yao.
“Mheshimiwa Mbunge kiukweli sisi
wakina mama tumekuwa tukiingia kwenye malumbano na familia zetu sababu kubwa ni
kutokupatikana kwa maji tunakuomba kama mwakilishi wetu utusaidie”Alisema Bi
Angelina.
Kutokana na Ombi hilo ,Mbunge wa
jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu,alisema kuwa wamepata Bilioni mia moja
kutoka serikali ya India ambazo zimekopwa na serikali ili kusaidia upatikanaji
wa maji katika maeneo ambayo yamekuwa na changamoto.
“Mkandarasi anatarajia kuanza
kazi mwezi wa saba kwa kuakikisha anasambaza maji kwenye maeneo ambayo
yameonekana kuwa na changamoto kubwa ya maji kwenye halmashauri ya mji wa Geita
kwa hiyo niwahakikishie wananchi kuwa swala hili tunashughulika nalo na
tutaakikisha changamoto hii tunaimaliza”Alisema Kanyasu
Aidha kwenye mkutano huo,meneja
ufundi wa Gewasa,Isaac Mgeni ,akisema kuwa tatizo la kukatika kwa maji linatokana na
matengenezo ya miundo mbinu ambayo imekuwa ikitumika kutibia maji pamoja na kukatika kwa umeme kuwa kwenye matengenezo lakini hata hivyo bado
wapo kwenye jitihada za kukomesha kero hiyo.
Diwani wa Kata ya Nyankumbu
Michael Kapaya amewataka wananchi hao
kuwa na subira kwani serikali imejipanga kutatua changamoto zinazo wazunguka
hususani za miundo mbinu.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: