Hii inaitwa noa bongo, ilikuwa ni zamu ya mwandishi wa Tanzania Daima Mkoani Geita Victor Bariet akirushiwa mpira na hapa akifunguka alichojifunza kwenye mafunzo hayo.
|
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Wakili James Marenga, akitoa somo |
.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. Wakimsikiliza Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, hayupo ichani.
|
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kwa umakiiini zaidi. |
Mwakilishi wa Metro Fm Mwanza, Alphonce Kapela, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
|
Picha ya pamoja, waandaaji wa mafunzo, wakufunzi wa mafunzo pamoja na washiriki wa mafunzo ambao ni wanahabari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Geita na Simiyu.
|
Mafunzo hayo ya siku mbili tangu jana, yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, yakilenga kuwajengea wanahabari uelewa juu ya Sheria Mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na Kanuni zake za mwaka 2017 ili kuwasaidia katika utendaji wa majukumu yao bila kukinzana na sheria na kanuni hizo.
Pamoja na mambo mengine, washiriki wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) Tanzania, wamefundishwa sheria na taratibu za kuandika na kuripoti habari/ makala kuhusu haki za binadamu kwa kuangazia sekta ya afya juu ya habari na makala za magonjwa ya kuambukiza kama HIV/Ukimwi ambapo wameahidi kuifikisha elimu hiyo kwa wenzao na pia kuitumia vyema katika kuboresha utendaji kazi
Post A Comment: