Wananchi
wa kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita wameiomba Serikali
kufanya maboresho ya kituo cha magari ya abiria kutokana na
kutokuwepo na kituo rasmi cha kuegesha magari hali inayowalazimu
madereva wa vyombo hivyo kuegesha magari pembezoni mwa barabara
pamoja na kandokando ya makaazi ya watu.
Hali hiyo
imekuja mara baada ya storm fm kuzuru kata ya Mganza na kujionea
madereva wakiegesha magari kandokando ya makazi ya watu huku wengine wakiegesha
pembezoni mwa barabara kwa lengo la kusubiria watu wanao safiri.
wakizungumza baadhi ya wakazi wa maeneo hayo ambapo magari
hayo huegeshwa bi, mwima masatu , emanuel mpuya na wengine
wengi wameonekana kukerwa na hali hiyo ambapo wamedai kuwa ajali za
marakwamara zimekuwa zikijitokeza hususani kwa watoto wadogo kutokana na hilo
wanaiomba serikali kuhakikisha inatatua changamoto hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Bw. Emanuel mwita
amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa tayari suala hilo amelifikisha
halimashauri ya wilaya ya Chato na kufikia makubaliano ya kuanza ujenzi
huo mara moja.
Aidha Bwana Mwita amewaomba wananchi wake kuwa wavumilivu wakati
serikali ikiendelea na utaratibu wa kuanza ujenzi wa kituo kipya cha kuegesha
magari katika kata hiyo.
Post A Comment: