Mkuu wa wilaya ya Geita mwalimu Hermani Kapufi amewataka wananchi kuacha kujenga nyumba za makazi katika vyanzo vya maji na badala yake kuvilinda na kuvithamini ili visikauke.
Akizungumza na wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa
katoro hivi karibuni mkuu wa wilaya ya geita mwalimu hermani
kapufi amewataka watu walio vamia katika
maeneo ya serikali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji na kujenga nyumba za
makazi pasipo kufuata sheria na taratibu waondoke mara moja na kuya acha maeneo hayo yakiwa wazi.
Aidha baadhi ya wananchi katika eneo hilo Bw. Salmin godfrey na Mashaka yahaya wameeleza kuwa wamefurahishwa na hatua ya mkuu wa
wilaya ya kuzuia watu kujenga nyumba za
makazi katika vyanzo vya maji pamoja na katika taasisi za kiserikali kama shule
na hospital kwani kwa kufanya hivyo
nikuyafanya maeneo hayo kuwa huru
na salama .
Post A Comment: