Gaudencia Gibay ambaye ni Afisa Lishe wa Shrika lisilo la Kiserikali la IMA WORLD HEALTH akitoa mafunzo kwa maafisa Kilimo na Lishe ambao wanatoka kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Geita. |
Afisa Lishe kutoka Taasisi ya Lishe Nchini Bi,Mary Kibona akitoa semina juu ya namna ya kumtunza mama mjamzito na mtoto. |
Wanasemina wakisikiliza kwa makini kile ambacho kilikuwa kikielekezwa. |
Katibu tawala wa Mkoa wa Geita ,Selestine Gesimba akifunga mafunzo hayo uku akiwasisitiza wanasemina kutumia vyema kile walichofundishwa. |
Gaudencia Gibay ambaye ni Afisa Lishe wa Shrika lisilo la Kiserikali la IMA WORLD HEALTH akitoa maelezo ya chakula cha mfano cha mtoto kwa Katibu tawala wa Mkoa wa Geita ,Selestine Gesimba |
Joseph Machibya mwenyekiti wa mafunzo hayo akimshukuru Katibu tawala kwa kufika na kufunga mafunzo hayo. |
Godfrey Mbaruku ambaye ni Mratibu wa Mawasiliano Mradi wa Mtoto Mwerevu akitoa ufafanuzi juu ya semina ambayo wamewawezesha maafisa kilimo na lishe Mkoani Geita. |
Mkoa wa
Geita unakabiliwa na tatizo la udumavu kwa kiwango cha asilimia 40.5 ,na hii
inatokana na tatizo la baadhi ya kabila kuwa na unyanyapaa kwenye swala la
chakula kwa wakina mama wajawazito.
Akifunga
mafunzo ya siku tatu yaliyokuwa yameandaliwa
na shirika lisilo la kiserikali la IMA WORLD HEALTH kwa maafisa kilimo na watu wanausika na sekta
ya afya ambao wanatoka halmashauri tano zilizopo Mkoani Hapa,Katibu tawala wa Mkoa Huo,Selestine Gesimba amesema kuwa ni
vyema kwa watendaji hao wakatumia nafasi hiyo kuakikisha wanapambana na tatizo
la udumavu na kutoka kwenye asilimia iliyopo kwa sasa.
“Natoa
maelekezo kwamba kama wewe umeshiriki kikamilifu katika mafunzo haya basi ni
matarajio yangu kuwa nitaona mabadiliko makubwa katika jamii,na hivyo suala la
UDUMAVU litapungua kwa kiasi kikubwa Mkoani kwetu”Alisisitiza Gesimba.
Afisa Lishe kutoka taasisi ya chakula Lishe
nchini Bi,Mary Kibona ambapo ameelezea kuwa hali ya udumavu nchini hapa ni
kubwa kwani ni asilimia 34.5 ya watoto wanashida hiyo.
“Hali ya
UDUMAVU sio nzuri nchini kwetu hususani katika Mikoa ambayo inalima chakula kwa
wingi kwa Mfano,Kagera ,Mara na Geita ni miongoni mwa mikoa ambapo tatizo hili
ni kubwa sana”Alisema Bi,Kibona.
Baadhi ya
washiriki kwenye semina hiyo Bi
Magdarena Thomas na Joseph Machibya wameelezea kuwa jamii ambayo hipo Mkoani
Hapa bado ni tatizo kwani wengi bado awajatambua swala la rishe kwa mtoto na
mama mjamzito.
Kutokana na
hali ilivyo ya Tatizo Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na
Serikali ya Uingereza kupitia shirikia la IMA world Health chain ya mradi wa
Mtoto Mwerevu,limeonelea kuanzisha mpango huu kwaajili ya kupambana na Tatizo
la UDUMAVU.
IMEANDALIWA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE
Post A Comment: