CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU TANZANIA (OJADACT) TUNALAANI MAUAJI YA ASKARI 7 MKOANI PWANI.

Share it:
Image result for EDWIN SOKO

Chama tumepokea kwa masikitiko makubwa mauaji ya askari saba yaliyotokea Mkoani pwani.

Kitendo hicho kwetu ni uhalifu kwa kuwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Nchi ibara ya 14 kila mtu ana haki ya kuishi.

Mauaji ya askari wetu ni unyama mkubwa uliofanywa na watu wachache wasio na nia njema ya Taifa hili,na wanaotaka kuona taifa linaingia kwenye umwagaji dawa pasipo sababu ya msingi.

Kazi ya Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake ni kuwalinda raia na mali zake,licha ya jukumu hilo kuna watu wachache ambao wamekuwa kikwazo kwa jeshi hilo kutekeleza majukumu yake.

OJADACT , tunalaani vikali kitendo hicho na kutoa pole kwa Mkuu wa jeshi wa polisi Nchini kwa yote yaliyotokea.

Tunawaomba watanzania wote kutojihusisha na vitendo vya kihalifu badala yake tujenge umoja na mshikamano wa taifa na kupiga vita uhalifu Nchini.

Mwisho tunaviomba vyombo vya habari kuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kupiga vita vitendo vya kihalifu vinavyoendelea hapa Nchini.

Edwin Soko
Mwenyekiti

Share it:

matukio

Post A Comment: