MGODI WA DHAHABU WA GEITA (GGM) WAONYESHA TEKNOLOJIA ZA KISASA ZA UOKOAJI KWENYE MAONYESHO YA USALAMA NA AFYA MJINI MOSHI

Share it:




Wataalamu wa ukoaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) wakitoa somo la namna ya kumuokoa mtu aliyepata ajali kwenye Gari kwenye maonyesho ya OSHA yanayofanyika mjini Moshi.

Bw Isack Senya(katikati) akiongea na Vyombo vya Habari kuhusu ushiriki wa Kampuni ya Geita Gold Mine kwenye maonyesho ya Afya na Usalama mahala pa Kazi.






Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) umeshiriki maonyesho ya afya na usalama mahala pa kazi yanayoratibiwa na wakala wa usalama na afya mahala pa Kazi(OSHA)mjini Moshi ambapo wameonyesha teknolojia na mifumo mbalimbali ya Afya na usalama mahala pa kazi.

Maonyesho hayo ni shamra shamra za kuelekea tarehe 28 April 2017 ambapo Tanzania itajumuika na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Usalama na Afya mahala pa Kazi.

Mrakibu wa Usalama mahala pa Kazi kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Isack Senya amesema kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita umetoa kipaumbele kikubwa kwenye suala la usalama mahala pa kazi na ndiyo maana kwa zaidi ya miezi kumi na saba Mgodi haujapata ajali iliyosababisha kushindwa kurudi kazini siku iliyofuata `(lost time injury incident).


“Mwaka jana kwenye maonyesho ya OSHA,GGM ilipewa TUZO kama Kampuni kinara inayoongoza kufanya vizuri kwenye masuala ya usalama mahala pa kazi. Siri yetu kubwa ni Tunu muhimu ambayo tumejiwekea”Usalama kwanza kwenye shughuli zetu zote”a lisema Bw Senya na kuongeza kuwa Kauli mbiu ya maonyesho haya mwaka 2017 ni “ongeza wigo wa ukusanyaji na utumiaji wa data za usalama na afya” kuchangia utekelezaji wa lengo namba nane la maendeleo endelevu linalosisitiza kazi na staha na ukuaji uchumi.


Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) umeweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji na utumiaji wa data za usalama na afya ili kuepuka ajali na vifo kwa wafanyakazi.Bw Senya amezishauri Kampuni zingine pia ziige mfano mzuri wa Kampuni ya Geita Gold Mine ambayo ina utaratibu wa kufuatilia kwa ukaribu kila data wakati wa ajali au tukio linaloweza kuleta madhara.

Kampuni ya Geita Gold Mine hivi sasa pia imeshika nafasi ya pili kwenye suala la afya na usalama kazini katika Migodi 20 inayomilikiwa na Kampuni tanzu ya Anglo Gold Ashanti.
Share it:

habari

Post A Comment: