KIKOSI cha timu ya Simba kimeendelea kujifua kwa nguvu wakijiandaa na mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam utakaofanyika mwishioni mwa wiki hii.
Jumamosi ya April 29, ni nusu fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho la Azam HD baina ya Simba na Azam itakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Kwa sasa Simba wapo Morogoro wakijiandaa na mchezo huo ambapo chini ya Kocha Joseph Omog na Jackson Mayanja kimeamua kujichimbia huko kwa ajili ya kuwapa muda wa kupumzika wachezaji wake na kuwapa mbinu mpya mbalimbali.
Hii inakuwa ni mechi ya ushindani mkubwa sana kwa timu hizi mbili zikikutana kwa mara ya tatu ndani ya msimu mmoja ambapo katika michezo miwili ya awali ila mmoja akishinda mchezo mmoja.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa wachezaji wana ari kubwa sana na wako vizuri na wanaamini watapigana mpaka mwisho ili kupata ushindi kwenye mchezo huo.
“Huu ni mchezo muhimu sana kwetu, ni muhimu kupata ushindi ili tuweze kuingia fainali ya kombe la Shirikisho na wachezaji wana ari kubwa sana ya ushindi na wameahidi kupambana mpaka mwisho,”amesema Ally.
Mpaka sasa Kikosi cha Simba kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao wanatarajiwa kuukosa mcheoz huo ambao ni Hamad Juma na Jamal Mnyate.
Post A Comment: