Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga Akizungumza na wananchi kwenye viwanja vya CCM Kalangalala Mjini Geita. |
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza mgeni Rasimi. |
Katibu wa TUGHE Mkoani Geita Ethel Kahuluda akielezea changamoto ambazo zinawakabili watumishi kwenye shughuli ambazo wanazifanya. |
MKUU wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amekemea vikali baadhi ya watu wanaoendelea kuwatumikisha watoto kwa kufanya kazi ngumu na zenye ujira mdogo.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa kauli hiyo katika kilele cha sherehe ya wafanyakazi Duniani, ambayo mkoani Geita imefanyaki katika viwanja vya CCM Kalangalala Mjini humo, huku kitaifa maadhimisho hayo yakifanyika Mkoani Kilimanjaro.
Kyunga alisema vitendo hivyo ni kinyume cha sheria, ambapo ameviagiza vyombo husika ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali, viongozi wa dini, vyombo vya dola na asasi zinazoshughulikia haki za watoto kushilikiana kwa dhati kukomesha jambo hilo.
“Nitumie fursa hii lukemea baaadhi ya watu wanaowatumikisha watoto kuwafanyisha kazi ngumu zenye ajira mdogo na usiokidhi haja zao, tunastahili kushirikiana kupiga vita kwa nguvu zote…haki ya motto ni kupata elimu na kulelewa katika mazingira bora na si vinginevyo,’’alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Pia RC Kyunga hakuacha kugusia suala la matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu kwa wafanyakazi wote na wananchi, ambapo alipiga marufuk na kusema si jambo zuri kwa matumizi ya madawa ya kulevya kwani zina athari kubwa kiakili, kiafya na kuathiri ustawi wa jamii.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Post A Comment: