YANGA 2 VS KAGERA 1

Share it:
Image result for YANGA VS KAGERA


KADI Dk 87, Mbaraka Yusuf analambwa kadi nyekundu hapa. Anatoka nje hapa, inaonekana alishindwa kuzithibiti hasira zake.

Dk 85 sasa, Yondani yuko chini anatibiwa pale baada ya kupata dhoruba
Dk 82, Fakhi analala na kuokoa mbele ya Msuva na kuwa kona, inachongwa lakini haina msaada.

 SUB Dk 78 Chirwa anakwenda benchi upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony.

Dk 76 kwa mara nyingine, Kaseja anaonyesha umahiri wa juu kabisa baada ya kuruka na kudaka vizuri kabisa hapa kichwa kilichopigwa vizuri kabisa hapa na Tambwe 
Dk 74 Mbaraka Yusuf anaangushwa nje kidogo ya 18 ya Yanga. 

Kagera wanapiga faulo lakini haina nguvu 
Dk 72 Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi kabisa lakini Kaseja anaonyesha umahiri hapa, anapangua vizuri kabisa 
Dk 69, Mbaraka Yusuph anaachia mkwaju mkali hapa, lakini Yanga wanaokoa na Themi Felix anashindwa kuuthibiti mpira.


Dk 68 Ame Ali hapa alikuwa anaingia vizuri lakini anaangushwa hapa na mwamuzi anasema ni faulo 
Dk 67 Kaseja analazimika kuukoa mpira kwa kichwa baada ya kutaka kuonyesha manjonjo.

Dk 65, Kaseja anadaka hapa mbele ya Tambwe ambaye alikuwa na nafasi nzuri ya kuandika bao la tatu 
SUB Dk 64 anatoka Kessy kwa upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Juma Abdul wakati Kagera wamemuingiza Japhet Makarai 'Balotelli' akichukua nafasi ya Edo Christopher 
Dk 61, Fakhi na Kaseja walijichanganya hapa na mpira unatoka na kuwa kona


SUB Dk 58 Kagera wanamtoa Babu Seif na nafasi yake inachukuliwa Anthony Matoghola 
DK 57, Msuva anachuana vikali hapa na Fakhi hata hivyo anamzuia 
Dk 55, Niyonzima anaachia mkwaju mkali hapa lakini Kaseja anadaka kwa ubora kabisa 
GOOOOOOOOOO Dk 52, krosi safi kabisa hapa ya Niyonzima, Chirwa anaunganisha vizuri kabisa na kuandika bao la pili
Dk 48, krosi nzuri ya Kessy inatua kwa Msuva lakini anashindwa kuunganisha 
Dk 45 Yanga wanaanza kwa kasi kubwa wakionekana wamepania kupata bao la pili 



MAPUMZIKO
-GOOOOOOOOOOOO Mbaraka Yusuf anaachia mkwaju mkali kabisa na kuandika bao safi kwa Kagera  
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yondani analala na kuokoa mpira hapa dhidi ya Ame Ali
Dk 43 Kakolanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju mkali wa Mbaraka Yusuf na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina manufaa
Dk 41 Mwinyi Haji anamuangusha Mangoma ambaye alijaribu kumtoka hapa


GOOOOOOOOOOOO Dk 39 Msuva anaruka na kupiga kichwa safi akiunganisha kona ya Mwashiuya na kuiandikia Yanga bao safi kabisa
Dk 35, Mangoma nje ya 18, anaachia mkwaju mkali hapa, hata hivyo hakulenga lango 
Dk 31, Fakhi anautoa mpira nje tena na kuwa kona. 

Inachongwa vizuri hapa, Mwashiuya anajaribu kufanya yake lakini anakosea
Dk 30 Kessy anaachia mkwaju mkali kabisa lakini hakuwa amelenga lango


Dk 26 sasa, Yanga wanaonekana kujipanga vizuri kupeleka mashambulizi mengi lakini Kagera Sugar wanaonekana wakiwatuliza Yanga
Dk 22, Yanga wanapata koa nyingine baada Mangoma kupiga fyongo. 

Inachongwa kona lakini Kagera wako makini 
Dk 20, Chirwa akiwa ndani ya hatua tatu, anapiga mpira kabla ya kuingia wavuni unaokoleewa na Kavila na kuwa kona. Inachongwa lakini Kagera wanaokoa hapa 
Dk 16, Fakhi anafanya kazi ya ziada, analala na kuokoa mpira dhidi ya Chirwa na kuwa kona. Inachongwa vizuri lakini Yanga wanaokoa hapa 
Dk 15, Mbaraka Yusuf anamtambuka Cannavaro ambaye analazimika kumkinga na kumuangusha. 

Cannavaro ameonyesha uzoefu wake maana ilikuwa ni hatari 
Dk 13, krosi safi ya Kessy, Msuva anaachia bunduki kali, lakini hakulenga lango. ilikuwa hatari hapa 
Dk 10 sasa, Kaseja yuko chini pale akitibiwa. Inaonekana alipata maumivu wakati akijaribu kuokoa 
Dk 10, Yanga wanafanya shambulizi jingine kali kabisa hapa, lakini Kaseja anaruka kama nyani na kuokoa, lakini amegongwa na kuanguka chini  
Dk 6, krosi safi ya Kessy hapa lakini Fakhi anaruka vizuri na kuokoa hapa 
Dk 4, krosi nzuri ya Niyonzima anajaribu hapa Chirwa lakini inashindikana 
Dk 1, Yanga imeanza kwa kasi ikiwa imepania kufunga bao la mapema
Share it:

michezo

Post A Comment: