DOTO APOKELEWA KWA SHANGWE KUBWA BULANGWA-BUKOMBE

Share it:


 Wakazi wa Kata ya Bulangwa wakimpokea Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa jumbe mbalimbali.




 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya wanabukombe baada ya kuwasili mkutanoni





 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisaini katika Kitabu cha wageni na wapembeni yake ni Mbune wa Jimbo la Geita Mjini Mhe. Constatine Kanyasu.







 Katibu wa CCM (W) Bukombe Aveline Ngwada akizungumza katika mkutano huo.



 Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Bukombe na Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe. Safari Nikas Mayala akizungumza na wakazi wa Bulangwa




 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM(W)Bukombe Mhe. Zakaria Bwire akitoa pongezi kwa Rais Magufuli namna anavyoiendesha Nchi ya Tanzania




 Mbunge wa Jimbo la Geita  Mjini  Mhe. Constatine Kanyasu akiwasalimia wanabukombe


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM(W)Bukombe Mhe. Zakaria Bwire akisema neno baada ya Dickson Bagamba(kulia) kuamua kwa dhati kurudisha kadi ya Chama ACT Wezalendo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM



Picha ya baadhi ya waliouliza maswali katika Mkutano wa  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko





 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko  amewaomba wananchi wa Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ndiye mwakilishi wao kwa sasa  huku akiwaomba na kuwasihi wazidi kumuombea Rais Magufuli kwa kazi ngumu anayoifanya ya kuwatetea wanyonge pamoja na maslahi ya Taifa kwa ujumla.

 Biteko amebainisha hayo katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa Jimbo hilo la Bukombe kwa kumuwezesha kumchagua kwa  kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani.

Aidha,Doto aliwaomba wananchi wa Kata Bulangwa  kuwa na subira kwani atahakikisha Umeme wa gridi ya Taifa inapita katika vijiji vyote vya Wilaya ya Bukombe uku akiwabainishia mradi uliokwisha haukua  Mradi wa REA hivyo amewaeleza mpango wa sasa ni kupata umeme wa uhakika hadi kwenye baadhi ya vyanzo vya maji ili kupunguza na changamoto ya maji na kwa sasa tayari ameliombea hilo na litatekelezwa muda wowote kuanzia sasa.

Mbali na hilo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo la Bukombe  kutojenga katika miundo mbinu ili wakati wa serikali kufanya maendeleo kusiwe na kikwazo cha kuwaathiri wananchi hao. 


  Mhe. Doto Mashaka Biteko pia mbali na kutoa shukrani kwa wapiga kula wake hao, pia alipata wasaha wa kusikiliza kero za wananchi huku akipokea kero zao hizo ambapo ameeleza kuwa atazifanyia kazi

Wananchi waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji,kusumbuliwa na wahifadhi na kuuliza nini hatima ya serikali juu ya milioni hamsini za kila kijiji, barabara mbovu pamoja na Ukosefu wa Umeme.
Share it:

habari

Post A Comment: