WACHIMBAJI WADOGO WAVAMIA MGODI WA BUCKREEF GEITA.

Share it:
Eneo la Mgodi wa Bakrif ambalo limevamiwa na wachimbaji wadogo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akizungumza na Baadhi ya wachimbaji wadogo kwenye mgodi wa Bakrif  uliopo kwenye Kata ya Lwamgasa

Wachimbaji wadogo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Geita wakati alipokuwa akitoa maagizo.

Afisa Madini wa Mkoa wa Geita Ally Said Ally akielezea juu ya leseni ya mgodi huo

Zaidi ya wachimbaji mia moja (100) wa kata ya Lwamgasa Wilayani Geita wamevamia kwenye maeneo ya Mgodi wa Buckreef na kuanza shughuli za uchimbaji kwa madai kuwa mwekezaji amemaliza muda wake ana hataki kuwapatia fidia ya maeneo yao.

Akizungumzia  juu ya tatizo ambalo limepelekea wachimbaji kuvamia Mwenyekiti  wa chama cha Mapinduzi  CCM Kwenye kata Hiyo Edward Kiswaga ,amesema kuwa kuna watu ambao walitathiminiwa na walitakiwa kulipwa na kwamba takribani miaka minne wamekuwa wakizungushwa juu ya kupatiwa fidia zao.

“Tuliwai kuja na Mheshimiwa Kalemani wakaahidi kwamba watajenga barabara na kutoa huduma kwa wanajamii wa Lwamgasa  lakini nimekuwa nikifuatilia kwa Mheshimiwa Minda na nina wauliza kwa nini hamtekelezi ahadi zenu wamekuwa wakisema Mkurugenzi yupo Canada huku kuna watu ambao tayari wameshatathiminiwa wanatakiwa kulipwa fedha zao”Alisema Kiswaga

Kutokana na madai ya kutokulipwa fidia ya maeneo yao Meneja wa Mgodi wa Buckreef  , Peter Zichovu amesema kuwa walikuwa na mpango wa kuwalipa watu hao lakini tatizo kubwa ambalo lilionekana ni watu kuongezeka na kwamba walikuwa wana mpango wa kufanya tathimini na kuwalipa watu hao ambao wamekuwa na madai ya fedha zao.

Kutokana na maelezo hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alikwenda kutatua  shida hiyo kwa wananchi amesema kuwa tarehe 15 watakutana yeye na naibu Waziri kwenye eneo hilo na kwamba amewapa wachimbaji hao siku tatu (3) kufanya shughuli za uchimbaji na baada ya hapo wayaachie maeneo hayo hadi pale uwamuzi utakapofikia  wa maeneo hayo.

Eneo la Buckreef   lina leseni ya uchimbaji Mkubwa na kwamba leseni hiyo inamilikiwa  ubia kati ya shirika la madini la Taifa Stamico pamoja na kampuni ya Tanzamu na kwamba leseni hiyo inadumu miaka kumi (10) na kwamba imekwisha kumalizika lakini tayari  wamekwisha fanya taratibu  za kubadilisha (kulinew) leseni hiyo ingawa bado haijawekewa saini  na Waziri mwenye  dhamana.


IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

Share it:

habari

Post A Comment: