MKAPA AKABIDHI THEATRE NA KUWATAKA VIONGOZI KUBUNI MIRADI ILI WAWASAIDIE WANANCHI:

Share it:
.Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamina Mkapa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la upasuaji katika kata ya nkoma walayani Itilima mkoani simiyu, kulia kwake ni waziri wa Afya, Maendeleleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu na kushoto kwake ni balozi wa japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida.
Rais wa awamu ya Tatu Benjamini mkapa akikagua vitanda ndani ya jengo la upasuaji baada ya ufunguzi wake katika kituo cha Afya nkoma wilayani Itilima mkoani Simiyu leo.


Rais Mtaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa akipata maelelzo toka kwa mtaalamu wa wa afya jinsi kituo hicho kitakavyotoa huduma kwa wananchi mara baada ya kufungua jengo la upasuaji katika kituo cha afya nkoma wilayani itilima mkoani simiyu.
 Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga akiongea na wananchi wa kata ya Nkoma baada ya ufunguzi wa jengo la upasuajia katika kituo cha afya nkoma.



(Imeandaliwa na  COSTANTINE MATHIAS, Simiyu)

RAIS wa Awamu ya tatu Benjamini mkapa amekabidhi jengo la upasuaji na kuwataka watanzania kujitegemea katika kubuni miradi ambayo itasadia jamii kwa lengo kuondokana na utegemezi wa mataifa tajiri .

Mkapa amesema kuwa kama taifa tusitarajie mataifa tajiri kuja kutuinua kama sisi wenyewe tumekaa kwa kuwa hiyo ni dhana potofu inayorudisha nyuma juhudi za maendeleo kwa wananchi.

Rais Mkapa ameyasema hayo wakati akifungua jengo la upasuaji katika kata ya Nkoma wilayani Itilima mkoani Simiyu huku akiwasisitiza viongozi wa serikali kubuni miradi ili kujiendeleza kama wanavyofanya nchi ya Japan.

Jengo hilo ambalo limejengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na nchi ya Japan limegharimu milioni 270 ambapo wakinamama wajawazito, watoto na wagonjwa walikuwa wakiipata huduma hiyo umbali wa kilomita 40.

Alisema kuwa mijadala mingi inayoendelea kwa sasa ni ya kisiasa na siyo ya kuleta maendeleo hivyo jamii na taifa kwa ujumla wanao wajibu wa kuongeza ari katika kujiendeleza na kujitegemea kwa wasomi, wananchi na wafanyakazi.

Aliongeza kuwa kila mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha taifa linajitegemea na kuwaletea wananchi wake maendeleo, huku akiwataka wasomi na wafanyakazi kuendesha midahalo na makongamano ya kuhakikisha nchi inajitemegea.

“ kila siku utasikia watu wanadai haki, makongamano, midahara ya kudai haki, swali la kuwauliza wao je wametimiza wajibu kama watanzania? Maana hakuna haki bila wajibu, ni lazima kubadilika na kuendesha makongamano ya kuonyesha nchi itajitegemea vipi” alisema Mkapa.
 
Aidha aliongeza kuwa ili kuweza kujitegemea ni lazima kila mtanzania akatimiza wajibu wa kufanya kazi kama Rais Magufuli anavyosema, huku akitoa mfano katika nchi ya Japani kuwa wananchi wake jambo la kwanza ni kufanya kazi.
 
“ kama tunatarajia mataifa kuja kutuinua wakati sisi tumekaa, ni dhana potofu, vuongozi tubuni miradi ili tujiendeleze na kujiletea maendeleo sisi wenyewe, kaama nchi ya Japani wanavyofanya” alisema Mkapa.
 
Aliongeza kuwa toka utawala wa Baba wa Taifa na sera ya Chama cha Mapinduzi toka zamani ilikuwa ujamaa na kujitegemea, jambo ambalo ameeleza lazima yatekelezwe kwa kila mmoja katika kutimiza wajibu kwa nafasi yake.
 
Akiongelea Jengo hilo Mkapa ameishukuru nchi ya Japana ambao walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo kupitia taasisi ya Mkapa foundation, huku lengo likiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.
 
“ Nchi yetu bado tunakabiliwa na changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, Nchi ya Japan wametoa msaada huo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hii, taasisi ya Mkapa foundation itaendeleza ushirikiano na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za afya” alisema Mkapa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa vifo vitokanavyo na uzazi kati ya wakina mama 100,000 vimepungua kwa mwaka hadi 559 kwa mwaka ambavyo husababishwa na kuvuja damu, maambukizi ya maradhi na uzazi pingamizi.

Mwalimu alisema kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto za afya hasa huduma ya upasuaji ili kufuikia 2020 angalau 50% ya vituo vitoe huduma ya upasuaji ili kuokoa maisha ya wagonjwa.

Alisema kuwa kufikia mwezi Desemba mwaka huu katika jengo hilo serikali italeta mashine ya ultra sound ili kuweza kukidhi mahitaji ya wagonjwa, na pia wataajiri zaidi ya watumishi wa afya 3000 na kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya.

Katika hatua nyingine Mwalimu amesema kuwa serikali imetoa bei elekezi kwa dawa za binadamu ili hata mwananchi mwenye kipato kidogo aweze kumudu gharama za matibabu huku akisisitiza kuwa dawa siyo bure.

‘’bei za dawa siyo bure na wananchi mnatakiwa kuchangia dawa katika vituo na zahanati…bei za dawa zimepunguzwa tangu jana na tunataka wananchi waone upungufu huo katika madawa ya kupata dawa hizo’’ alisema Mwalimu

Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga alisema kuwa pamoja na kukamilika kwa jengo hilo upungufu wa watumishi bado ni changamoto kubwa wajibu wa serikali ni kuajiri watumishi ili waeze kuhudumia wananchi.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika ufunguzi huo walisema kuwa jengo hili limeongeza faraja kwa akinamama wajawazito na wagonjwa kwani wengi wao walikuwa wakifia njiani wakati wakisafirishwa kwenda Bariadi kupata huduma ya upasuji.

Mary Kasuka mkazi wa Mwalushu alisema kuwa awali walikuwa wakipata taabu sana kupata huduma ya upasuaji na wanaishukuru taasisi hiyo kwa kuwasogezea huduma ya upasuaji na kuitaka serikali kuhakikisha huduma ya maji inapatikana wakati wote kituoni hapo.

Share it:

habari

Post A Comment: