RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

Share it:
jak1
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
jak2 jak3
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.
jak4 jak5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
jak7 jak8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
jak9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,  Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
jak10 jak11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kumaliza ziara yake Chato mkoani Geita ambapo alikabidhi nyumba 50 zitakazotumika katika sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera.
jak12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Anna Mkapa.
jak13
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akiangalia hotuba yake kabla ya kuhutubia wananchi mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
jak14
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
jak15
 Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
jak16
Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya Alizeti  (Double Refine) kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan. PICHA NA IKULU
Share it:

HABARI PICHA

Post A Comment: