Mheshimiwa Doto Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha magorofani kwenye mkutano wa uzinduzi wa barabara.
(PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE0)
Wanakijiji
wa kijiji cha Magorofani Kata ya Igulwa
Wilayani Bukombe Mkoani Geita ,wamelazimika kufunga barabara kwa kutumia Ndoo za
kuchotea maji wakati wa ziara ya Mbunge
wa Jimbo Hilo,Mh Dotto Biteko kwa madai ya kuwa na changamoto ya ukosekanaji wa
maji kwa muda mrefu.
Mh,Dotto
ambaye alikuwa kwenye moja kati ya shughuli za kukagua na kujionea ujenzi wa
barabara pamoja na kufungua kijijini hapo amekutana na kundi la wanawake pamoja
na watoto wakiwa wamefunga barabara na wakiomba kutatuliwa adha hiyo ambayo imekuwa ikiwasumbua ya kukosekana kwa maji.
Wakizungumza
kwa Nyakati tofauti na mtandao wa
Madukaonline baadhi ya wananchi wa kijiji hicho,Faines James,Mirembe
Ngussa na Happynes Hai,wameelezea kuwa
wamekuwa na shida ya maji kwa muda mrefu na kwamba kilichimbwa kisima lakini
nacho hakitoi maji hivyo uamuzi wa kuweka ndoo kwenye barabara walitaka
kumuonesha mbunge wao namna ambavyo wamekuwa wakipata shida ya maji.
Aidha kwa
Upande wake Diwani wa Kata Hiyo ,Richard Mabenga amekiri kuwepo kwa tatizo la
maji na kwamba hadi sasa kuna visima
vitatu tu ambavyo vinahudumia kata nzima na watu ambao wanategemea visima hivyo
ni wakazi elfu kumi na tisa mianane (19800).
Kutokana na
tatizo Hilo ambalo wananchi wameliwakilisha kwa Mbunge wao,Mhandisi wa Mji wilayani hapo Aaron Swai ,amesema kuwa
serikali kwenye bajeti yake ya mwaka 2017/18 imepanga kujenga mtandao wa maji
safi na salama kwenye kata hiyo ambao utahudumia watu zaidi ya elfu kumi na nane na kwamba watu zaidi ya
asilimia 81 watakuwa wanapata maji safi na salama.
Hivyo
kutokana na hali hiyo Mbunge Dotto Biteko amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa
wana miradi kumi ya maji na kwamba moja kati ya kata ambayo imetengewa fedha
nyingi za kujenga mradi wa maji ni pamoja na kata hiyo na kwamba watahakikisha
wanaleta maji kwenye kata hiyo na kwamba mwisho wa mwezi huu mkandarasi atakuwepo
kwenye kata hiyo.
Kata ya
Igulwa inawakazi zaidi ya elfu 22,000 na ambao wanapata maji safi na salama ni
aslimia kumi tu ambayo ni sawa na wananchi 2,000.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: