Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akisalimiana na watumishi pamoja na wakuu wa idara mbali mbali Mkoani humo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akimkabidhi hati ya pongezi Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akionesha Hati ya pongezi ambayo amepatiwa na Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akiagana na watumishi. |
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimkabidhi Mkuu wa Mkoa mambo muhimu ambayo ameyaandika wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi. |
Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa huo pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM). |
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa kwenye ofisi yake kwaajili ya kuanza shughuli rasmi.(PICHA NA MADUKA ONLINE)
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi amewataka watumishi na wakuu wa wilaya Mkoani humo kuwatumikia kikamilifu wananchi wenye matarajio makubwa kwa serikali yao.
Mhandisi Lughumbi aliyasema hayo alipozungumza na watumishi na kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa huo katika hafla ya kukabidhiwa ofisi na Mtangulizi
wake Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliyestaafu nafasi hiyo.
Alisema
amefika kwenye Mkoa wa Geita kufanya kazi hivyo watumishi wote wawajibike
kuchochea maendeleo kwa kasi ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu.
“Nimeingia
katika Mkoa huu kama mlivyonikaribisha mmenikaribisha nimekuja kufanya
kazi nimekuja kutumika nimetumwa kuwa
mtumishi kwa mwendo tulionao hatuna muda wa kupumzika ni kipindi cha mageuzi
lazima tugeuze kitu kigeuzike watu wajue tumegeuza hata wanaofuatilie waone mambo yapo sawa sawa ukione maendeleo yanakimbia ujue uku
kulipokuwa kunachelewa vilikuwa vipindi
vigumu vya matengenezo”Alisema Lughumbi.
Pia
amezungumzia tatizo la uduni wa miundombinu ya elimu na shida ya maji
inayoendelea kuwasumbua wananchi wa Geita.
“Wakina mama
bado wanandoo kichwani katika Mkoa tupo asilimia hamsini upatikanaji
wa maji safi na salama kuna watu
wamecheza na fedha ya umma maji hayajaja
tangu miaka ya sabini meja jenerali wewe ulikuwa mpole mimi naenda kwenye sait nitakuwa mkali kidogo hasa ambao
wanacheza na mali ya umma”Alisisitiza Lughumbi.
Mkuu wa Mkoa
mstaafu, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alisema kwa sasa anakwenda
kupumzika na kuwataka wanaobaki kulitumikia taifa wafanye kazi kwa weledi na
kasi inayoendana na ile ya Rais Dr John Magufuli.
Mkoa wa
Geita ni Kati ya Mikoa ambayo ilianzishwa mwaka 2012,na wakuu wa Miako ambao
wamepita hadi sasa ni watatu ,Magalula Said Magalula,Fatuma Mwasa na Meja
jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu hivi karibuni na kumpisha
,Mhandisi Robert Lughumbi.
Post A Comment: