NAIBU WAZIRI LUGOLA AZINDUA OPERESHENI YA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI NZIMA.

Share it:






TAMKO LA MHE.  KANGI ALPHAXARD LUGOLA. (Mb.)
NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MUUNGANO NA MAZINGIRA JUU YA OPERESHENI MAALUMU IJULIKANAYO  KWA JINA LA "TUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA -TUSALIMIKE"ALILOLITOA KATIKA  ENEO LA  TANDALE KWA MTOGOLE WILAYA YA KINONDONI
 DAR ES SALAAM, 30/10/2017.


Harakati mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuweka Majiji, Halmashauri na Miji, yetu safi,  ikiwa ni pamoja na matamko mbalimbali ya viongozi wakuu hapa nchini. Aidha, Halmashauri za miji na majiji zimekuwa zikiendesha kampeni za usafi kwa kuweka siku maalumu za kufanya usafi wa mazingira na pia kusimamia sheria, kanuni, miongozo na sheria ndogo izinayohusu mazingira.



Nguvu za ziada zinahitajika ili Halmashauri ziweze kuchukua hatua za dhati za kudhibiti taka pamoja na kuhakikisha sheria ndogo na sheria nyingine zinatekelezwa kwa vitendo ili kuhakikisha usafi wa mazingira unasimamiwa ipasanyo na kuhakikisha mazingira yanayotuzunguka yanakuwa masafi.



Pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali bado usafi wa mazingira hauridhishi, taka ngumu katika maeneo mbalimbali kama maeneo ya makazi na maeneo ya biashara hazizolewi kwa wakati, utunzaji wa mifereji ya maji ya mvua na utunzaji wa bustani za burudani haujafikia kiwango kinachostahili, taka bado zinatupwa ovyo kando kando ya barabara na chini ya madaraja na pia taka kutumika kama njia ya kuziba makorongo na kuzuia mmomonyoko wa kingo za mito katika makazi ya watu. Tabia hii imesababisha kuziba kwa mifareji iliyotengenezwa kwa gharama kubwa wakati wa mvua na kusababisha mafuriko ambayo yamepelekea nyumba nyingi kujaa maji na kuharibu mali za wananchi na hata kusababisha vifo.




Katika kuhakikisha kuwa suala la kampeni ya usafi ni endelevu na yenye mafanikio, leo nataka tuzindue  operation maalumu ya kuzibua mitaro yote nchini, operation hii itakuwa endelevu kwa kila Mkoa, Wilaya , Halmashauri, Kata, Mtaa, Kijiji na Kitongoji. Tutahakikisha kuwa watendaji wote kulingana na sheria ya mazingira na kamati zao wanahakikisha kuwa uchafunzi wa mazingira sasa basi. Hatuwezi kuona nchi inaendelea kuwa katika hali ya uchafu wa aina hii,  wananchi wanakufa kwa kipindupindu na magonjwa mengine wakati watendaji wapo katika ngazi zote kwa mujibu wa sheria.



Operation hii itakuwa ya miezi miwili kuanzia tarehe 1 Novemba hadi tarehe 30 Desemba 2017  na haiondoi maelekezo ya awali ya kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. Baada ya tahere 30 Desemba 2017 ukaguzi wa utekelezaji wa agizo hilii utafanyika nchi nzima kuanzia Januari 2018 Operation hii tutaisimamia sisi ndani ya Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Maafisa mazingira wa Mikoa na Wilaya  pamoja na watendaji wote hadi katika ngazi ya kitongoji na kila mtu atawajibika kwa nafasi yake.



Asanteni kwa kunisikiliza


Share it:

habari

Post A Comment: