Akizungumza kutokea ndani ya Hifadhi ya Serengeti, ambapo
amefanya ziara ya kushtukiza na kuuzunguka mpaka wote wa Mashariki
ambapo hifadhi ya Serengeti inapakana na Pori Tengefu la Loliondo, lenye
mgogoro wa muda mrefu, Dkt. Kigwangalla ameagiza Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi, kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa
Wanyama Pori, Prof. Alexander Songorwa mara moja. Ametoa sababu kuwa ni:
1. Tuhuma za kuhujumu Serikali kwa kutoa taarifa za siri za
Serikali kwa vyombo vya habari na kutunga taarifa zenye kulenga
kuchochea mgogoro wa Loliondo. (Jana usiku zilizunguka taarifa kwamba
Dkt. Kigwangalla yupo na msafara wa gari mbili binafsi (private) njiani
kwenda Loliondo na kwamba atalala Hotel ya Acacia iliyopo Karatu. Na leo
msafara wake umekuwa ukifuatiliwa na watu wasiojulikana ambapo kila
hatua aliyofikia ilikuwa ikiripotiwa kwenye mtandao, hali ambayo
imetishia usalama wa kiongozi huyo).
2. Waziri Kigwangalla amesema Mkurugenzi huyo amekuwa
akifanya kazi kwa maelekezo ya muwekezaji wa Kampuni ya Utalii wa
Uwindaji ya OBC (maarufu kama kampuni ya kiwindaji ya wafalme wa Dubai).
Kampuni hii imekuwa ikihusishwa na kashfa kwa miaka zaidi ya 26.
3. Aidha Prof. Songorwa amekuwa akihusishwa na kashfa ya
kushiriki kugawa vitalu vya uwindaji kinyume cha sheria. Wiki mbili
zilizopita Waziri Kigwangalla alisitisha mchakato wa kuhuisha leseni za
uwindaji uliofanywa na Prof. Jumanne Maghembe, aliyekuwa waziri wa
Maliasili na Utalii kwa tuhuma za rushwa na kukosekana uwazi kwenye
mchakato huo.
Pia ameelekeza mchakato wa kugawa vitalu sasa ufanywe kwa
njia ya mnada.
Pia, ameelekeza TAKUKURU waanze kuchunguza kashfa za rushwa
dhidi ya kampuni ya OBC na waanze kwa kumhoji bwana Mollel (Mkurugenzi
wa OBC) ambaye amekuwa akijigamba kila kona kuwa alimhonga Maghembe dola
200,000, huyu kijana Kigwangalla dola 100,000 inamtosha! Dkt.
Kigwangalla amesisitiza hahongeki na ndiyo maana jitihada za bwana
Mollel kumuona zimekwama, na hata alipotumiwa ujumbe kupitia watu wake
wa karibu alikataa.
Ili kuimarisha ulinzi wa mpaka wa Mashariki mwa Serengeti,
Waziri Kigwangalla amewaondoa Askari wote wa Kituo cha Geti la Kleins
kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji huyo ambaye ana mahusiano ya
Karibu na Prof. Songorwa, na alikuwa na mahusiano ya karibu na Prof.
Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na
Utalii wa zamani.
|
Navigation
Post A Comment: