Bill Gates ni mwanzilishi, mwenyekiti na mbunifu mkuu wa programu za
kampuni ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani,
inayoaminika kwa utengenezaji wa programu zilizo na nguvu na ubunifu
hali zikiwa bado zenye utumizi mwepesi.
Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu hamsini na tano katika nchi
themanini na tano. William Gates III H anajulikana kama Bill Gates
alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle
pamoja na dada zake wawili. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa
na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini
Seattle.
Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen
mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki. Hapo ndipo wakaanza kutumia
tarakilishi ndogo ya shule kujiendeleza ujuzi wao. Waliajiunga na
kampuni ya kompyuta malipo yao ikiwa ni kutumia tarakilishi yenye nguvu
zaidi.
Kazi yao ilikuwa ni kutafuta nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati
huohuo waliweza kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye
Chuo Kikuu cha Harvard Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo
kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya
kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800.Kampuni hiyo iliridhishwa na
kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa
leseni. Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha kampuni ya
Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu.
Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na
kujishughulisha muda wake wote katika biashara. Mapumziko yao yalikuja
walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika
katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza
kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo
wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka
ya 1980 na baadaye, Microsoft pia ilianza kutengeneza programu kama vile
neno sindikizi.
Microsoft ilitangaza mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao Windows
1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa na grafiksi bora na pia uliwezesha
kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati mmoja. Hata hivyo hakuwa bidhaa
nyingine iliyotolewa miaka MIWIli baadaye hadi mwaka wa 1985, kwa kuwa
ni programu chache zilizoweza kuendeshwa katika mfumo huu wa Windows
1.0. Hivyo mfumo huu mpya haukupata umaarufu vile.
Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya
Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya
Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa
umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika
historia ya Marekani. Katika mwaka wa 1990 Microsoft ikiongozwa na Bill
Gates ilitoa toleo jipya la Windows liitwayo Windows 3.0 na kuboreshwa
kiasi GUI.
Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya nakala milioni kumi,
likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na makundi ya kazi
ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana na mafanikio yao ya
maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine ya Windows 95 ikifuatiwa na
Windows 98, 2000, Millennium Edition na toleo la sasa Windows XP. Kila
toleo jipya lilipotolea kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu
katika soko la hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile
Microsoft Office, michezo n.k.
Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu tajiri duniani myenye thamani
ya wastani wa dola bilioni arubaini na sita. Bill Gates pia ana maslahi
katika biashara nyingine akiwa na nafasi nyingi za uwekezaji na vyeo
katika kampuni tofauti ikiwemo Corbis Corporation, Berkshire Hathaway
Inc, Teledesic Corporation. Mwaka wa 1998 Gates alijitoa jukumu lake
kama Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Microsoft na kuzingatia maendeleo ya
teknolojia na bidhaa mpya. Bill Gates alifanya ndoa na Melinda French
Gates mwaka wa 1994 nawakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na
Fibi.
Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya
kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates
Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni tatu nukta
mbili kuboresha afya duniani, dola bilioni mbili kuboresha fursa ya
masomo kwa familia zisizojiweza.
Zaidi ya hayo limeweza pia kuchangia dola milioni mia nne sabini na saba
kwa miradi ya jamii na zaidi ya dola milioni mia nne themanini na nane
kwa miradi maalum na kampeni za kuhamasisihwa kila mwaka. Ubunifu wa
Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi
ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.
Navigation
Post A Comment: