Mtuhumiwa Bw,Saayai Petro ambaye anashitakiwa kwa kumuoa Binti wa miaka 16 akiwa amekamatwa. |
Mzee Kashirima Kashimba ambaye ni Baba wa Binti huyo akiwa amekamatwa baada ya kuwakimbia askari. |
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akielezea hatua za kushikiliwa mzazi wa Binti huyo na dada yake na mwanaume ambaye alikuwa amemuoa. |
Ikiwa
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza wanafunzi kupelekwa shule na
kupatiwa Elimu Bure Hali imekuwa ni Tofauti kwa Binti mwenye umri wa miaka 16 ambaye anatoka Kata ya Kanyara Wilayani Geita amejikuta
akilazimishwa kuozeshwa na mzazi wake wa kiume baada ya kumaliza darasa la saba
na kufaulu kuendelea na masomo ya kidato cha
kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kasamwa.
Binti
huyo Alifaulu mwaka 2017 kuingia kidato cha kwanza mwaka 2018 katika shule ya
sekondari Kasamwa lakini hakuwahi kuhudhuria masomo hata siku moja.
Baba
mzazi aliyejulikana kwa jina la Kashirimu Mashimba amepokea posa ya Ng’ombe
watano kutoka kwa Saayai Petro aliyetaka kumuoa binti mwenye umri wa miaka 16.
Kaimu
afisa mtendaji wa Kata ya Kanyara Bw,Augustino Kazanza amesema kuwa walibaini
kuwa binti huyo amehozeshwa kutokana na kupata taarifa kwa wananchi wenye
mapenzi mema.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Mji Mhanidisi Modest Aporinaly amesema kuwa bado kuna changamoto
ambazo zimeendelea kujitokeza kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni
kutokana na baadhi ya watu kuendelea kuendekeza mali na kuacha kuwapa Elimu
wasichana.
Mkuu
wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amelaani kitendo hicho na kuwataka
wananchi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa dhidi ya watu ambao wanawahozesha
wanafunzi
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema hadi sasa
wanawashikilia watu watatu ambao ni
Dada,Baba pamoja na kijana ambaye ndiye muoaji
Ikumbukwe
tu kuwa Mkoa wa Geita katika takwimu za wanafunzi watoro inashika nafasi ya
Pili kwa Skondari asilimia 8.1 na
msingi asilimia 3.1
Post A Comment: