Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa Nje ya vibanda vyao baada ya kufungwa na Halmashauri ya Mji wa Geita. |
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamekaa wakitafakari hatua ya kufungiwa kwa vibanda vyao hali iliyowapelekea kushindwa kuendelea na Biashara. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola akizungumza na wafanyabiashara baada ya kufika na kujionea hali hiyo. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akizungumza juu ya hatua ambayo imechukuliwa ya kuvifungia vibanda ambavyo avijalipa kodi ya elfu therasini. |
Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bashiri Mhoja akizungumzia kifungu ambacho kinamhurusu mkurugenzi kuvifungia vibanda vya wafanyabiashara hao kutokana na kukiuka makubaliano. |
Zaidi ya vibanda
Hamsini (50) vya Wafanyabiashara
kwenye Stendi kuu ya Mkoa wa Geita vimefungwa kwa madai ya kukaidi agizo la kulipa kodi iliyo pangwa na
Halmashauri ya Mji wa huo.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara hao Bi. Mwajuma Hassani na Bw. Sadick Mbido wameilalamikia Halmashauri ya mji wa Geita kwa
kitendo cha kukiuka makubaliano ya mkataba kwani kwasasa walikuwa wanalipa kodi
ya Tsh. elfu kumi (10,000) kwa mwezi
ambapo ilikuwa ni ya mkataba unaoisha mwaka 2020 na kwamba ni jambo lililowashangaza kutokana na
kulazimishwa kulipia kiasi cha Tsh. Elfu thelathini (30,000).
Hata hivyo Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Stendi hiyo, Bw.
Hamis Ayaki amesema kuwa kitendo ambacho
kimefanyika ni ukiukwaji wa makubaliano na kipo kinyume na makubaliano na kwamba ameelezea namna ambavyo mkataba
ulikuwa ukisema.
Kwa upande wa Katibu wa Wafanyabiashara Bw. Isack
Shoo ameiomba Serikali kuwasaidia kutokana na wao kuendelea kulipia mapato ya Serikali
na kwamba wana familia ambazo zinawategemea hivyo kufanya hivyo ni sawa na
kuwaonea na kuwanyima haki zao za msingi.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao baada ya kufika
na kujionea kufungwa kwa Shughuli zao Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa
Geita, Bw. Leornad Bugomola amewataka kuwa watulivu na kwamba suala lao
litashughulikiwa kwa wakati na watarudi kuendelea na shughuli zao.
“Ndugu zangu kwanza niwashukuru maana mmekuwa
watulivu mmenipigia simu nimekuja na ndio tunataka namna hii sio kujichukulia
hatua mkononi mimi nawaomba muwe watulivu ikiwezekana niondoke na viongozi wenu
hili tufuatilie suala hili na likikamilika watawaletea majibu” Alisema
Bugomola.
Kutokana na malalamiko hayo Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Aporinaly alisema wameshakaa na wamiliki wa Vibanda na
wakaelewana kuwa watalipa Tsh. Elfu thelathini hivyo kitendo ambacho wanakiona ni ukiukwaji
wa makubaliano baina ya wamiliki wa Vibanda na Wapangaji.
Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bashiri Mhoja amesema kuwa
ndani ya mkataba kipengele namba tatu
(3) kinamruhusu Mkurugenzi kufanya
mabadiliko baada ya kipindi cha miaka mitatu kutokana na mfumuko wa Bei.
Post A Comment: