WAZIRI MKUU AGUSWA NA HOJA YA MBUNGE PENEZA

Share it:
WAZIRI Mkuu, Kassim Majali, ameshauri Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Upendo Peneza, kukaa na Waziri wa Fedha na Mipango na yule wa Tamisemi, kushauriana njia bora ya kuhakikisha taulo za kike zinapatikana kwa bei nafuu ambazo wanafunzi walioshindwa kwenda shule wakati wa hedhi watazimudu.

Kauli hiyo ya Majaliwa imekuja baada ya Pendeza kutaka kauli ya Serikali juu ya kondoa kodi kwenye taulo hizo, akisema baadhi ya wanafunzi kutoka kaya masikini wamekuwa wakishindwa kuhudhuria mawasomo wawapo kwenye hedhi kwa sababu ya kushindwa kumudu taulo hizo za kujisitiri.

“Kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha inaondoa vikwazo vyote kwenye elimu, na Waziri wa Tamisemi alishaelekeza zile Sh 10,000 na Sh 20,000 zinazopelekwa kama ruzuku kwa shule za msingi na sekondari zitumike kununua taulo hizo, lakini ikizingatia fedha hizo ni kidogo, kwanini sasa Serikali kwenye sheria ya fedha inayokuja isiondoe kodi kwenye taulo hizi ili wanafunzi kutoka kaya masikini waweze kuzimudu,” aliuliza Peneza wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema “Serikali ina utaratibu wake wa kuondoa kodi kwenye bidhaa zinazoleta tija ikiwamo uliyoisema mheshimiwa Mbunge, kwa kuwa serikali imeanza kutoa fedha kama ulivoeleza, Wizara ya fedha na Waziri (Tamisemi)  wataona namna mtakavyokaa kuona jinsi ya kupunguza bei kwenye vifaa ulivyoeleza.”

Share it:

habari

Post A Comment: