Serikali Mkoani Geita imewaonya
watu au vikundi ambavyo vitaonekana kuvunja amani ya Mkoa na kwamba mkoa upo imara katika kudumisha
suala la ulinzi na usalama.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na vikosi
vya ulinzi na usalama nje ya ofisi za mkoa.
Amesema ni vyema kwa jamii
ikatambua kuna
walinzi hivyo wanawajibu wa kutii sheria bila ya kushuru kwenye maeneo ambayo wanaishi.
Aidha Mkuu wa mkoa Ameongeza
kwa kusema anatambua changamoto walizonazo Askari katika utendaji wao wakazi
hivyo ilikuwafanya wapate nguvu za kufanya kazi tayari wamekwisha kuanza
mchakato wa ujenzi wa Nyumba 100.
Mkuu wa Mkoa amesema kumekua na imani potofu za mauaji ya vikongwe,
Maaskari na walinzi kwa imani ya kupata mali kupiti damu ya watu hao,hivyo ameagiza
vikosi hivyo kupinga na kupambana vikali na vitaa hiyo ili kutokomeza mauwaji
hayo.
Mkoa wa Geita Upo
kwenye Kampeni ya Wiki mbili ambayo inaitwa TAFAKARI YA ULINZI NA USALAMA MKOA
WA GEITAinayotarajia kumalizika tarehe
28 ambayo inalengo la kudumisha amani ya Mkoa huo.
Post A Comment: