MWENYEKITI WA KIJIJI MKOANI GEITA AHUKUMIWA KWA MAKOSA YA RUSHWA

Share it:
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilombero 1 kata ya Lwamgasa Wilayani Geita ,Bw Mahano Bitendo Bihogo akiwa nje ya mahakama kabla ya kusomewa mashitaka ambayo yalikuwa yakimkabiri.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilombero 1 kata ya Lwamgasa Wilayani Geita ,Bw Mahano Bitendo Bihogo ,akiingia ndani ya mahakama kwaajili ya kusikiliza mashitaka ambayo yalikuwa yakimkabili.

 Mwendesha mashitaka wa Takukuru ,Bw Kelvin  Murusuri  akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ambazo zimechukuliwa mahakamani dhidi ya mwenyekiti wa Kilombero 1.

Mkuu wa Takukuru Mkoani Geita,Bw Thobias Ndaro,akitoa ufafanuzi juu ya hatua ambazo wameendelea kuzichukua dhidi ya watu ambao wamekuwa wakiendekeza vitendo vya Rushwa Mkoani humo. 
Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Geita  imemuukumu Mwenyekiti wa kijiji cha Kilombero 1,Bw Mahano Bitendo Bihogo kwenda jela miaka mitatu kutokana na kukutwa na hatia ya makosa matatu  ambayo ni kushawishi na kupokea hongo kinyume na kifungu cha 15(1)(a)na(2)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu cha sheria na kanuni za adhabu sura ya 16 R:E 2002.Katika shauri la jinai Na.114/2018.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya  mwendesha mashitaka wa Takukuru ,Bw Kelvin  Murusuri  Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Geita,Kaliho Mrisho amesema mahakama imemkutana na hatatia mshitakiwa  na kwamba mahakama imejiridhisha pasipokuwa na shaka yoyote na ushahidi ulioelezwa na mwendesha mashitaka ,Bw Murusuri baada ya mtuhumiwa kukiri kutenda makosa hayo.

Mwendesha mashitaka wa Takukuru Bw,Kelvin Murusuri amesema  mwenyekiti  huyo Aliomba  na kupokea fedha kiasi cha milioni moja kutoka  kwa mwekezaji Hussein Mwananyanzara  ili awapatie posho wajumbe wa serikali ya kijiji kwa lengo la  kukaa kikao ambacho kililenga kumjadili na kumpitisha kuendelea na shughuli zake.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea kabla ya kutolewa adhabu  alijitetea kuwa anao watoto na mke na wote wanamtegemea ,kutokana  na utetezi huo mahakama ilimpa adhabu ya kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya laki tano kwa kila kosa na kwa makosa yote alitakiwa kulipa milioni moja na nusu ,Mwendesha Mashitaka hadi anaondoka mahakamani mtuhumiwa alikuwa ajalipa faini hiyo na amepelekwa gerezani.


Mkuu wa Takukuru Mkoani Geita,Bw Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuendelea kufichua uonevu na kushiriki vyema kwenye mapambano dhidi ya vitendo  hivyo  kwa kutoa taarifa mbali mbali za vitendo vya rushwa katika Nyanja zote ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na kwa kufanya hivyo wananchi watakuwa wameshiriki kutokomeza vitenndo vya Rushwa.

Share it:

habari

Post A Comment: