MZEE WA MIAKA 69 AOA BINTI WA MIAKA 13 GEITA

Share it:
Mzee John Mkubila akiwa ameshikiliwa na Moja kati ya wananchi ambao wanaishi mtaa wa Mwembeni Kata ya Nyankumbu Mjini Geita baada ya kukamatwa ameoa binti wa miaka kumi na tatu(13).

 Mzee John Mkubila akizungumza juu ya suala la kumuoa Binti wa miaka kumi na tatu wakati alipokuwa amekamatwa na jeshi la polisi jamii.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza juu ya hatua ambazo zimechukuliwa na jeshi la Polisi kutokana na tukio la mzee John Mkubila.

Jeshi la Polisi Mkoani Geita Linamshikilia Mzee  wa miaka  sitini na tisa (69) kwa kosa la kumuoa Binti wa Miaka kumi na tatu(13)  ambaye anatokea kitongoji cha Rwenge Kijiji cha Bugalama.

Mzee huyo ambaye anajulikana kwa jina la John Mkubila ambaye ni mkazi wa mtaa wa mwembeni kata ya Nyankumbu mjini Geita amekiri kumuoa binti huyo kwa makubaliano ya mzazi  wa binti huyo kuwa awe anamsaidia kazi za nyumbani kutokana na mke wake kuwa na majukumu mengi ya kibiashara hali ambayo imepelekea  kujikuta mzee akikosa huduma za msingi na kuamua kumuoa binti huyo.

“Nilionana na Baba yake nikamwambia kuwa kwa sasa umri wangu umekwenda naweza kupata binti mdogo wa kunisaidia maana kwangu nina mke ila ana majukumu mengi hivyo najikuta nashindwa kufanya shughuli zingine Baba yake akaniambia sawa ndio akawa amenipa huyu ambaye kwa sasa ni Mke Mdogo”Alisema Mzee Mkubila.

Aidha kwa upande wa Binti huyo amekiri kuolewa na mzee huyo  kutokana na  na  Baba yake mzazi kumlazimisha.

“Mimi nilikataa kuolewa Baba yangu ndiye ambaye alinilazimisha niolewe kutokana na kwamba  nimemaliza shule ya msingi ila mimi sikuwa tayari kuolewa kutokana na umri wangu kuwa mdogo”Alisema Binti.

Hata hivyo kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye ofisi za polisi jamii kwenye mtaa huo wamesikitishwa na kitendo hicho na kuitaka jamii kubadilika na kuachana na desturi ambazo zimeendelea kuwakandamiza watoto wa kike .

Kamanda wa Polisi Mkoani Humo Mponjoli Mwabulambo  amesema nyuma ya tukio kulikuwa na mapatano baina ya wazazi wa mtoto na huyo mzee  kama mahari ilitolewa lakini pia uchunguzi unafanyika na utakapokamilika wote watafikishwa mahakamani kwa kuwa ni kosa la kisheria kujamiana na mtoto mwenye  umri wa chini ya miaka kumi na tano(15). 


Share it:

matukio

Post A Comment: