Nyumba ikiwa imeezuliwa paa na kuanguka kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha Mkoani Geita.
Mvua
zinazoendelea Kunyesha Mkoani Geita zimesababisha maafa ya vifo vya watu saba
(7) watano wakitokea kwenye halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale na
wawili kwenye halmashauri ya Mji wa Geita.
Watu hao wamefariki kutokana kujaa maji
mto ambao upo kwenye mpaka wa Wilaya ya Nyang’whale na Sengerema huku mtu mmoja akiagukiwa na
ukuta wa Nyumba na mwingine akifariki kutokana na kusombwa na maji .
Akizungumza kwa njia ya Simu na mtandao huu Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale
Hamim Gweyama amesema hadi sasa mwili
ambao umetambuliwa na ndugu ni mmoja na
kwamba wanaendelea na jitihada za kutafuta miili mingine kwenye Mto huo.
Aidha kwa upande wake Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la
zima Moto na uwokoaji Mkoani Humo Stanley Paschal akizungumza na waandishi wa habari amesema
watu hao wawili miongoni mwao ni mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye
anajulikana kwa jina la Aneth Juma na Mzee Vicent Kipili ambaye aliangukiwa na
ukuta ,huku akiwataka wananchi kuwa waangalizi wa watoto wao kwenye kipindi
hiki cha msimu wa mvua.
Kwa upande wa Mashuhuda wa ajali ya Mtoto huyo
Bi,SCOLA SANGA NA LUNYIRI TEKANISA ambao
ni wakazi wa Mtaa wa Kivukoni Kata ya Nyankumbu wamesema kuwa walimuona mtoto
huyo akielea kwenye mtaro ndipo walipochukua jukumu la kumsaidia kumtoa na
walipomtoa walimkuta amekwisha kufariki.
Ikumbukwe kuwa mamlaka ya hali ya hewa hivi karibuni
imetaja mikoa ambayo itapata mvua kwa wingi ikiwemo na Mkoa wa Geita na
kuwataka wananchi ambao wanaishi kwenye maeneo ya mabonde kuchukua taadhari
mapema kwani mvua hizo zitaendelea hadi mwezi wa tano.
|
Post A Comment: