Baadhi ya wanaume wakiwa wamekaa wakisubilia taratibu za mazishi.
NA,MADUKA ONLINE ,GEITA
Wanaume wa
mtaa wa Buyegule kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji wa Geita
wamelazimisha Wanawake kuchimba kaburi la Marehemu Mkangiko Vigume kwa madai
Marehemu alifariki katika mazingira ya kutatanisha na kudaiwa Wanawake
wanahusika.
Imezoeleka kuwa kwenye jamii zetu wanaume ndio wanahusika wakuu
wa kufanya shughuli za uchimbaji wa kaburi na kubeba mwili wa
marehemu lakini kwenye mtaa huo hali imekuwa ni tofauti kutokana na madai ya
wanaume kulalamika kuwa wameendelea kupoteza maisha kwenye mazingira ya
kutatanisha na kujikuta wakiendelea kuisha na kuelezwa kufanya hivyo ni adhabu tosha kwa wanawake
ambao wamekuwa na tabia za kishirikina.
Wakizungumza kwa vipindi Tofauti na mtandao huu kwenye familia ya mzee Kangeko Vigume ambaye
amefariki kutokana na kuugua ghafla wamesema kuwa tukio hilo la kufariki
mwanaume sio la kwanza na kwamba hadi sasa kuna wanaume 7 wamepoteza maisha
kwenye mazingira ya kutatanisha .
“Kiukweli
sisi tumeumia sana kutokana na matukioa haya kuendelea kujirudia mara kwa mara
kwenye mtaa wetu sisi wanaume ndio ambao tumekuwa tukifa jambo la kushangaza
wao awafi wakifa ni magonjwa hila sisi ni ghafla”Alisema Mussa John.
“Jambo la
kusikitisha watu ambao tunawazika wamekuwa wakirudi na kutungongea hodi na uku
sisi tunajua tumewazika hili ndilo linatushitua zaidi sisi kama wanaume wa mtaa
huu”Alisema Mzee Kahema Msabira.
kwa upande wao wanawake wamesema kuwa kitendo ambacho
kimefanywa na wanaume wa mtaa huo sio kitendo kizuri kwani walitishwa na
kuambiwa kuwa wasipofanya shughuli ya kuchimba kaburi wataadhibiwa kwa kuchapwa
viboko kila mmoja.
“Sikutaka
kufanya shughuli hii ya kuchimba kaburi lakini jambo la kusikitisha
nimelazimishwa tu sisi wanawake tunaonewa sana kwani akuna wanaume
wachawi”Alisema Bi,Frola Nyanda.
Mwenyekiti wa mtaa huo,Bw,Andrew Barnabas amesema alishindwa
kuzuia wananchi kufanya kitendo hicho kutokana na wengi wao kutokusikiliza hoja
yake na kuamua kujichukulia maamuzi wao wenyewe.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amesema watakwenda
kwenye mtaa huo na kukutana na wananchi waweze kuwaelimisha ikiwa ni pamoja na
kuwachukulia hatua watu ambao wamehusika kuhamasisha suala hilo.
Pamoja na wanaume kuzika wamewataka wanawake hao
kujua kuwa hilo ni onyo na kwamba ikitokea Mwanaume mwingine kufariki kwenye
mazingira ya utata hawatashiriki kwa shughuli yoyote ile ya kuzika.
|
Post A Comment: