Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga akitangaza hatua zidi ya watumishi saba ambao wamekutwa na tuhumza za utoro kazini pamoja na wizi. |
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakiwa kwenye kikao cha tatu cha baraza hilo. |
NA,MADUKA ONLINE
Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Geita imewafukuza kazi
watumishi saba kutokana na kuwa na makosa
ya utoro kazini , Udanganyifu na wizi wa fedha na rasilimali za umma
ikiwa ni pamoja na Kushindwa kuwasilisha
mapato ya serikali na Kutokuwajibika.
Mamlaka ya Baraza la Madiwani imepewa nguvu ya kisheria
kuwawajibisha watumishi wa Halmashauri isipokuwa walimu na wale wanaoteuliwa na
Mhe. Rais au Waziri mwenye dhamana kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma
Na.8 ya mwa ka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.19 ya mwaka
2002, kifungu cha 6 (6).
Akitoa adhabu hiyo kwenye ukumbi wa Mikutano Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo Elisha Lupuga amesema
Kwa mujibu wa kanuni ya 42(2) na kanuni ya 43(2) ya Kanuni za Utumishi
wa Umma za mwaka 2003, aina ya makosa na adhabu zimeainishwa katika nyongeza
Na.1 na nyongeza Na. 2. kwamba adhabu ambazo zimeainishwa ni pamoja na
kufukuzwa kazi ,kupunguziwa mshahara au
kushushwa cheo.
“Hivyo kamati imejiridhisha na kuona wanastahili adhabu ya
kufukuzwa kazi kutokana na kukiukwa sheria ya ajira”Alisema Lupuga.
Mwenyekiti Lupuga amewataka watumishi ambao ni watoro na si
waaminifU, waadilifu na wezi na hawana
nidhamu kwenye Utumishi wa Umma wajipange la sivyo hawatabakia kufanya kazi
ndani ya Halmashauri ya hiyo kwani Hawatavumiliwa kutokana na vitendo hivyo.
Hata hivyo kwa upande wake Diwani wa Nyawilemelwa,Method
Gaspeli amesema maamuzi ambayo yamechukuliwa na baraza hilo yako sawa kwani
yatawasaidia watumishi wenye tabia za namna hiyo kujirekebisha.
Sanjali na hayo Mkuu wa Mkoa Huo Mhandisi Robert Gabriel
amelitaka baraza hilo kuwa na mkakati wa kuainisha mradi kwa kila mwaka ambao
utasaidia kuingiza mapato kwenye halmashauri hiyo.
Post A Comment: