AJALI YA BASI YAUA MMOJA GEITA

Share it:
Basi la Kampuni ya Mkwema lililosababisha umauti wa mtu mmoja likiwa limepakiwa pembeni kwenye maeneo ya Nyankumbu mjini Geita.






Mtu mmoja ambaye amejulikana kwa jina la Maneno Eliasi mwenye umri wa miaka 18 amefariki dunia kutokana na ajali iliyoliusisha basi la kampuni ya Mkwema lenye namba za usajili T765 DCU aina ya TATA huku watatu wakijeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea kwenye Barabara ya soko la Nyankumbu Mjini Geita ambapo imeelezwa dereva  wa basi hilo alikuwa akijaribu kumkwepa mwanafunzi ambaye alikuwa akivuka hali ambayo ilisababisha  kushindwa kumudu gari hilo kutokana na kukata kona kubwa iliyosababisha kuwapalamia waendesha baiskali  wawili walio kuwa upande wa kulia.

Bi,Colenta Mapunda ambaye ameshuhudia ajali hiyo amesema gari hiyo ilikuwa ikijaribu kumkwepa mtoto ambaye alikuwa akivuka barabara ndipo ilipopoteza mwelekeo na kuwapalamia waendesha baiskeli wawili ambao walikuwa wakiendesha.

Aidha Bw,Yusuf Kagoma  ameiomba serikali kupitia kitengo cha askari wa usalama barabarabani kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya alama za barabarani kwani wengi wao shida kubwa inayowasumbua ni kutokujua kanuni zipi wanaweza kuzitumia pindi wanapokuwa kwenye maeneo ya watu wengi na kwenye vivuko.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo amewataja majeruhia wa Ajali hiyo kuwa ni Elia Antony ambaye alipata michubuko na kuumia mdomoni,na Mwingine ni Kalekwa Julius yeye alipata mshituko na  Elias Mzambia ambaye alizulika kwenye maeneo ya shingoni.

Kamanda Mponjoli amesema kuwa hadi sasa bado awajabaini chanzo cha ajali hiyo na kwamba wanawashikilia wafanyakazi wa basi hilo kwa mahojiano zaidi ,huku wakimtafuta dereva , Bw Charles Mtaluma ambaye alitoroka  baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Share it:

habari

Post A Comment: