Mkuu wa Takukuru Mkoani Geita,Thobias Ndaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati alipokuwa akitoa taarifa juu ya utekelezaji wa Taasisi hiyo Mkoani Humo. |
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa TAKUKURU wakati alipokuwa akitoa taarifa ya vitendo vya Rushwa kwa kipindi cha Julai 2017 na Aprili 2018. |
Bi,Flora Charles akizungumza juu ya suala la kupatiwa elimu na TAKUKURU. |
Katika
kipindi cha Julai 2017 hadi aprili 2018
taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa Mkoani Geita imepokea ujumla ya taarifa
323 za rushwa na makosa mengine.
Taarifa
zilizopokelewa zinahusisha sekta za serikali za mitaa kesi 74,ardhi 29,madini
28,ujenzi 28,elimu 25,afya 21,polisi 19,siasa 18,mahakama 14,fedha 12,mifugo
11,misitu 08,huduma za jamii 08,kilimo 7,biashara 6,uvuvi 5,mawasiliano 4 ,maji
3,utalii2 na nishati 01.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Mkuu wa TAKUKURU
Mkoani Humo,Bw ,Thobias Ndaro
amesema kuwa wamefanya uchunguzi wa awali na kwamba ofisi yake imefungua
jumla ya majalada ya uchunguzi 29, na jumla ya majalada 14 yamepelekwa kwa
mkurugenzi wa mashitaka(DPP) kwaajili ya kuombewa kibali cha mashitaka .
Aidha
ofisi hiyo imefungua kesi mpya 15 mahakamani kwa makosa mbali mbali ya rushwa
kutoka sekta ya Tamisemi,mahakama,vyombo vya habari na afya.
Na
kesi ambazo zimeendeshwa ni 38 mahakamani kati ya hizo zilizotolewa maamuzi n
inane (8)ambapo kesi nne(4)zilizoshinda na nne(4) zilishindwa.katika kesi zilizotolewa
hukumu,jumla ya washitakiwa watano walipatikana na hatia na kupangiwa adhanu ya
kutozwa faini.
Ndaro
ameongeza kwamba wameweza kufanikiwa kuokoa kiasi cha fedha taslimu milioni ,8.7 katika idara za afya ,Elimu na
maliasili na pia imeweza kuokoa fedha kwa njia ya udhibiti jumla y ash,milioni
5.5 ambazo zilitokana na vyama vya ushirika ,mahakama ,sekta binafsi na polisi.
Baadhi
ya wananchi ambao ni wakazi wa mjini Geita,weiomba taasisi hiyo kuendelea kutoa
elimu zaidi kwa wananchi kwani wengi wao bado awajawa na uelewa dhidi ya
mapambano ya Rushwa.
Miongoni
kati ya mikakati iliyonayo Takukuru Mkoani humo ni kutatua kero kwa wananchi
hasa katika maeneo ambayo yanaongoza kwa rushwa ikiwa ni pamoja na kufuatilia
kwa ukaribu maeneo ambayo yameendelea kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa.
Post A Comment: