Askofu wa Kanisa AIC Dayosisi ya Geita Mussa Magwesela akizungumza na wahumini wa kanisa hilo waliojitokeza kumpokea kwenye ukumbi wa Lenny Hotel Mjini Geita. |
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakimsikiliza askofu wakati alipokuwa akizungumza nao. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola akizungumza juu ya umuhimu wa wazazi kuwekeza kwenye Elimu. |
Wakazi wa Mkoani Geita wametakiwa kuwekeza kwenye elimu kwa
watoto wao ili kuwaandalia mazingira mazuri ya maisha ya baadaye na kukabiliana
na ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Hatua hiyo imekuja ni kutokana na baadhi ya wananchi kutoona
umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu kwa watoto wao na kuwatumikisha na hata
kuwaoza ili wajipatie kipato.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la
AIC Dayosisi ya Geita alipozungumza muda mfupi baada ya kuwasili mjini Geita
akitokea masomoni nchini Marekani.
Amesema jamii inapaswa kutambua kuwa ni muhimu ikawekeza
nguvu katika kuwaendeleza watoto wao kielimu na kujiendeleza wenyewe kielimu
kwa kuwa hata maandiko yanasisitiza suala la elimu.
“Kuwekeza kwenye elimu ni jambo la busara na la muhimu
kwenye jamii zetu na tunajua kuwa pasipo elimu kila jambo linaweza kuwa ni gumu
mimi nawashauri wazazi na walenzi kuonelea umuhimu wa kuwekeza kwenye suala
hili ambalo baadae litawasaidi pindi watakapokuwa wanaendelea na maisha ya
mbeleni”Alisisiriza Askofu Magwesela.
Sanjali na hayo ameitaka jamii pia kuwa na desrturi ya
kujenga upendo ikiwa ni pamoja na kuthaminiana na kuachana na tabia ya kujenga
chuki ambazo zinaweza kusababisha kuondoa amani baina ya mtu na mtu.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita Bw Leornad
Bugomola amesema elimu ni kitu cha msingi na haijali umri wa mtu na kwamba
pamoja na Mkoa kufanya vibaya kwa kushika nafasi ya pili kwa utoro kitaifa bado
umeendelea kufanya vizuri kwenye mitahani ya Kitaifa.
Mwl Pendo Greyson
amewasisitiza wadau wa elimu kushiriki kikamilifu kwa kuelimisha jamii kutambua
umuhimu wa elimu.
Post A Comment: