Diwani
wa kata hiyo Bw,Maisha Malando akielezea kero ya kutokukamilika kwa Bwawa la maji ya kijiji hicho.
Wakazi wa kijiji cha Nyisanzi kata ya Bwawani Wilayani Chato
Mkoani Geita wameiomba serikali kuingilia kati ujenzi wa mradi wa Bwawa la umwagiliaji kutokana na
kuchukua muda mrefu bila ya kukamilika hali ambayo imeendelea kusababisha
changamoto kwa wakulima ambao walikuwa wanategemea kufanya kilimo cha
umwagiliaji.
Suala hilo limeibuliwa
na diwani wa kata hiyo Bw,Maisha Malando wakati akizungumza kwenye
mkutano wa mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati ulio kuwa na lengo la kusikiliza kero za
wananchi na kisha kuziwakilisha Bungeni.
Diwani Malando,amesema ni muda sasa umepita tangu kukwama
kwa shughuli ya ujenzi na pia mkandarasi ambaye alikuwa akitekeleza mradi huo
amekwisha kuondoka kwenye eneo la ujenzi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji hicho Thobias Magombe
amesema kuwa wakati mradi huo unaanza wao kama serikali ya Kijiji awakuweza
kushirikishwa na kwamba waliwaona wakandarasi wakifika na kuendelea na majukumu
yao ya kazi hali ambayo pia iliwatia mashaka kwani awakuwa na aarifa juu ya
utekelezaji wa mradi huo.
Aidha mmoja kati ya wananchi wa kijiji hicho Bw,Mussa Saguda
ameelezea kuwa wamekuwa wakipata shida kubwa kutokana na kwamba walihaidiwa
pindi Bwawa hilo lingekamilika wangeweza kuwezeshwa kilimo cha uwagiliaji
lakini kwa sasa hali imekuwa ni tofauti na matarajio ambayo walitarajia kuyaona
kwenye kijiji hicho.
Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato Dkt, Medard Kalemani amewahidi
wananchi hao kufuatilia mstakabali wa Bwawa hilo kwenye wizara husika kutokana
na kwamba kazi hiyo ilikuwa ikisimamiwa na wizara ya maji.
|
Post A Comment: