WANAUME WALIO WACHIMBISHA KABURI WANAWAKE WAOMBA RADHI

Share it:
Baaadhi ya wanawake wa Mtaa wa Buyegule Kata ya Mtakuja wakiwa kwenye Kikao kilichokuwa na lengo la kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili dhidi yao.

Diwani wa kata ya Mtakuja Constatine Molandi akingumza na wananchi wa mtaa wa Buyegule juu ya hatua ambayo waliichakua ya kuwachimbisha kaburi wanawake.

Mmoja kati ya wanaume wa mtaa huo,Danford John akiomba radhi kutokana na tukio la kuwachimbisha wanawake Kaburi.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na  wananchi wa mtaa wa Buyegule huku akiwataka wale wote ambao wamehusika kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Na,Joel Maduka,Geita

Siku chache baada ya Wanaume wa Mtaa wa Bwihegule Kata ya Mtakuja wilayani Geita kuwapa adhabu Wanawake kuchimba Kaburi kwa madai ya kuhusika kuwaua wanaume, kutokana na hali hiyo wamejitokeza  kuomba msamaha kwa Serikali huku baadhi yao wakikimbia nyumba zao kwa hofu ya kukamatwa.

Akizungumza kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya jamii hiyo kuachana na mila potofu  kwa niaba ya wanaume wengine Bw,Danford Joseph amekiri kutenda kosa hilo na kwamba wanaomba wasamehe kwani kufanya hivyo wamekiuka kutokana na kutokuwa na ushahidi wa vitendo vya kishirikiana kwa wanawake hao.

“Kiukweli tumefanya makosa sanaa kwa kuwazushia wanawake kuwa ndio wanatuuwa sisi wanaume hivyo tunaomba kusamehewa kwani tulifikiria sivyo na tumeona sisi ndio wakosaji”Alisema Danford.

Hata hivyo Bi,Mariam Bahati ambaye ni moja kati ya wanawake waliochimbishwa kaburi ameelezea namna ambavyo waliweza kupatiwa adhabu hiyo kutoka kwa wanaume wa mtaa huo.

“Ilikuwa ni tarehe 21 mwezi wan ne wanaume walituita wanawake kikao na kuanza kujadili mambo mbali mbali lakini jambo la kushangaza walianza kusema kuwa sisi wanawake ndio tumekuwa chanzo cha wanaume kuuwawa mara kwa mara kijijini hapo hivyo wakatuambia kuwa leo mtafanya kazi ya kuchimba kaburi pamoja na kupika chakula tulikataa lakini mwisho ilibidi tukubali baada ya kushinikizwa na kutishiwa kuwa tutachapwa viboko”Alisema Bi,Mariam Bahati.

Diwani wa Kata hiyo,Bw Cosntatine Molandi amesikitishwa na kitendo hicho na kusema imekuwa  ni fedhea kubwa kwa wanawake kufanyiwa jambo la namna hiyo  na kwamba kitendo hicho ni cha kukemewa kwa nguvu zote na kila mtu.

Kufuatia maelezo hayo Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi  amewataka wale wote ambao wamehusika na kuwadharirisha wanawake kuhakikishwa wanakamatwa na hatua za kisheria zichukuliwe zidi yao huku akiwaonya wananchi kuachana na vitendo vya mila potofu katika wilaya hiyo.
Share it:

habari

Post A Comment: