WAZIRI JAFO AAGIZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BWANGA UKAMILIKE NDANI YA MWEZI MMOJA

Share it:
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita kwenye ukaguzi wa ukarabati wa kituo cha Afya Bwanga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Geita katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Mabweni ya wavulana ya shule ya Sekondari ya Magufuli iliyopo Wilayani Chato Mkoani Geita.

Majengo ya Upasuaji,Hodi ya Mama na Mtoto ,chumba cha kuhifadhia Mahiti yakiwa bado hayajakamilika kwenye kituo cha afya cha Bwanga.

Barabara yenye  kiwango cha lami inayojengwa mjini Geita ikiwa na urefu wa kilomita 1.2 

Majengo yanayojengwa kwenye ofisi za halmashauri ya mji wa Geita.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ametoa mwezi mmoja kwa Mhandisi wa Ujenzi wa   Halmashauri ya Chato mkoani Geita kusimamia ipasavyo na kukamilisha Ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya Bwanga ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kutoka serikali kuu. 

Waziri Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa wilayani Chato mkoani Geita katika ziara ya kukagua  miradi ya maendeleo.  Jafo amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho na ametoa siku 30 kazi zote ziwe zimekamilika.


Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Japhet Simeo amemweleza Waziri Jafo sababu za kuchelewa ni kutokana na kuwepo wakandarasi ambao walikuwa wakiingia kwenye vikundi na kusababisha ghalama za ujenzi kuwa juu tofauti na ujenzi ambao ulikuwa ukifanyika.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari ya kidato cha tano na sita ya Magufuli.Shule hiyo imeimarishwa miundombinu yake ya vyumba vya madarasa, vyoo, bwalo la chakula, pamoja na mabweni. 

Akizungumza shuleni hapo, Jafo amewapongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo ya Magufuli kwa kuwa miongoni mwa shule 25 bora nchini  kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017.


Waziri Jafo amewataka wanafunzi wa kidato cha sita mwaka huu kuweka jitihada zao kwenye masomo  ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri.

Sanjali na hayo waziri Jafo amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Nyakiling’ani  Constraction Limited ambaye anajenga barabara yenye urefu wa kilomita 1.2 kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo kwa kuweka taa pamoja na mifereji  hifikapo 15 mwezi wa July.

Waziri Jafo amemaliza ziara yake ya siku moja Mkoani Geita kwa kutembelea miradi ya shule ya sekondari ya magufuli,shule ya msingi ya Bwanga ,kituo cha afya Bwanga ,Ujenzi wa soko la Mkoa,Barabara ya Mjini Geita na Ujenzi wa Ofisi za halmashauri ya Mji wa Geita.Huku akiupongeza Mkoa huo kwa kusimamia vyema fedha za maendeleo zinazotolewa na serikali.



Share it:

habari

Post A Comment: