Mraibu wa Ukimwi na Kifua Kikuu Mkoani Geita,Dk Josph Odera akielezea madhara ambayo yanaweza kujitokeza enda mwanaume asipofanyiwa Tohara.
Tangu kuanza kwa
zoezi la Tohara Mkoa wa Geita watu 800
wamekwisha kupatiwa huduma hiyo huku Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume
wasiofanyiwa tohara ndio wanaopata maambukizi ya VVU kirahisi huku waliofanyiwa
wanajikinga kwa asilimi 60 kupata maambukizi mapya.
Kutokana na usafiri
wa pikipiki kutumiwa na abiria wengi kwenye maeneo ya starehe Intra Health
wameamua kutoa elimu kwa waendesha boda boda
Kwenye Mji mdogo wa Katoro hili kutambua umuhimu wa kufanya tohara na
kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi.
Akizungumza nje ya Ukumbi wa Msengenye Mratibu wa Ukimwi
Mkoani Humo,Joseph Odero amesema kuwa
Mwanaume
asihetahiriwa anahatari ya kumuambukiza mwenza wake wa kike anayeshirikiana na
ye tendo la ndoa saratani ya Mango wa kizazi.
“Lengo la kuja kwa
huduma hii ni kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa
yatokanayo na ngono hivyo kwa mwanaume ambaye hajatailiwa anahatari kubwa ya
kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi”Alisema Odero
Hata hivyo kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya ya Geita Raphael Mhana
amesema kuwa mji wa katoro ni kati ya miji ambayo inaongoza kwa kiasi kikubwa
cha maambukizi ya VVU ambapo imezidi takwimu za kiwilaya kwa kuwa na maambukizi ya juu
zaidi ukilinganisha na maeneo mengine.
Aidha baadhi ya wadau
ambao wamejitokeza kwenye mafunzo hayo wamesema kuwa wamenufaika kwa kiasi
kikubwa na kwamba wamehaidi kuwa mabalozi kwa vijana ambao bado hawajajua
umuhimu wa TOHARA.
Meneja Mradi wa Tohara
Paulo Mwakipesile amesema sababu za kuwajengea uwezo waendesha boda boda
ni kutokana na kwamba wamekuwa ni mihongoni kati ya watu ambao wanafanya biashara hiyo wakati wote na kwamba elimu
ambayo wamewapa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia watu wengi zaidi.
Elimu inaendelea
kutolewa Mkoa humo kwa lengo la kuhakikisha kila Mwanaume anafanyiwa tohara
kuepeusha madhara kwa jamii na familia kwa ujumla.
|
Post A Comment: