WAFANYABIASHARA WASHAURIWA KUOMBA MIKOPO GEITA

Share it:
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Hamim Gwiyama akikata utepe pamoja na meneja wa NMB kanda ya ziwa Abraham Augustino  (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Tawi la NMB Wilayani  Nyang'whale Mkoani Geita.

Jengo la NMB Wilayani ya Nyang'hwale.


Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini shughuli ya uzinduzi wa Tawi la NMB Wilayani Nyang'whale.

Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Hamim Gwiyama akitafakari jambo na meneja wa kanda ya ziwa wa NMB Abraham Agustino wakati wa shughuli za uzinduzi wa Benki ya NMB.

Meneja wa kanda ya ziwa wa NMB Abraham Agustino ,akizungumza juu ya msaada ambao wameendelea kutoa kwenye jamii ikiwa kama Benki iliyo karibu na jamii.

Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Hamim Gwiyama akizungumza na wananchi juu ya faida ambazo wanaweza kuzipata kutokana na kufunguliwa kwa tawi hilo.


 Wafanyabiashara wadogo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita wameshauriwa kutumia Benki kuomba mikopo itakayowasaidia kujiinua kiuchumi kupitia biashara zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya NMB wilayani humo, Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Hamim Gwiyama amesema anatambua umuhimu wa huduma za kibenki kwa kuwa ni kichocheo maendeleo ya uchumi kwa wananchi  hususani wanaojishughulisha na biashara ndogondogo.

Aidha ameiomba Benk hiyo kuongeza zaidi matawi ili kurahisisha huduma ya kifedha kwenye maeneo ambayo bado hayana matawi ya Benki hiyo.

Meneja wa NMB kanda ya ziwa Bw Abraham Augustino amesema wametoa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kituo cha afya cha Nyang’hwale vyenye thamani ya Sh Milioni 5 na Magodoro kwa ajili ya Hosteli ya wasichana wa shule ya sekondari Kakola .

Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo wamesema wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za kibenki na kwamba tawi hilo litawasaidia kutoa na kuweka fedha na kuondokana na safari ya kwenda mjini Geita.


Share it:

BIASHARA

Post A Comment: