MWALIMU AKAMATWA KWA KUJIHUSISHA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE

Share it:



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akifafanua juu ya hatua ambazo wamezichukua kwa mwalimu Noel Seleman ambaye anashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kutembea na Mwanafunzi wake wa Kidato cha Pili.

Binti ambaye amekutwa akiwa  nyumbani kwa Mwalimu wake ambaye jina lake tunalihifadhi.

Bw Francis Andrea ni mzazi wa Mwanafunzi akielezea kusikitishwa kwake na kitendo cha Mwalimu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Binti yake. 




Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Bugando Kata ya Nzera Wilayani Geita anashikiliwa na Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mwanafunzi wake wa kidato cha Pili.
Imeelezwa kuwa Mwl huyo Noel Seleman amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mwanafunzi wake kwa muda wa mwaka mmoja sasa.

Bw Francis Andrea ni mzazi wa Mwanafunzi huyo ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Mwl huyo huku akiiomba serikali imsaidie.

“Ni muda nilikuwa nikisikia kuwa anamahusiano na mwalimu lakini siku hiyo aliondoka asubuhi niliporudi Nyumbani nikamuuliza mama yake akaniambia alimtuma lakini jambo la kusngaza tangu saa nne hadi saa nane alikuwa ajafika nyumbani ndio nikachukua maamuzi ya kumwambia mdogo wake ambaye alikuwa naye kuwa dada yako yupo wapi alinipeleka na kunionesha mimi ilibidi nirudi na kuwachukua vijana sita na wanawake wane tukaenda kumkamata baada ya kumkamata tulimwita balozi wa eneo hilo akashuhudia uovu wa Mwalimu”Alisema Bw Francis.

Mama wa Mwanafunzi huyo Bi Joyce Katambi  amesema mara kwa mara amekuwa akimkanya binti yake kujihusisha na mapenzi akiwa bado anasoma lakini amekuwa amsikilizi hali ambayo imepelekea kujikuta akikamatwa na mwalimu wake.

Agdes Charles amesema amekuwa akimuona Binti huyo akija na kuondoka kwa mwalimu huyo na hata wanapomuzuhia amekuwa akiwatukana na kuwaambia waache kumfuatilia.

Balozi wa eneo hilo Bw Shaaban Majaliwa amesema  walipozungumza na mwanafunzi huyo alikiri kuwa na mhusiano na Mwl wake tangu akiwa kidato cha kwanza.

Kwa upande wake Mwanafunzi huyo mwenye miaka 17 alipohojiwa na mtandao huu  amekanusha kuwa na mahusiano na Mwl wake na kwamba alikwenda nyumbani kwake kumjulia hali baada ya kupata  taarifa kuwa amepatwa na ajali.

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Bw Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limelitokea tarehe 13 mwezi huu majira ya saa nane mchana na mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Hata hivyo Mzazi wa mwanafunzi huyo amedai kuwa kuna dalili za tukio hilo kutaka kupotoshwa ukweli wake ili haki isipatikane


Share it:

habari

Post A Comment: