AFIKISHWA MAHAKANI KWA TUHUMA ZA KUOMBA RUSHWA YA NGONO

Share it:


Mtuhumiwa akiwa nje ya mahakama.

Joseph Mgile akiwa ameweka pozi la kupigwa picha na waandishi  baada ya kamera kumzonga zonga.


Taasisi  ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) Mkoani  Geita imemfikisha mahamani mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu GGM Joseph  Mgile kwa kosa la  kuomba ruswa ya ngono wakati wa kutoa ajira ndani ya mgodi huo.


Wakisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Geita Ushindi Swaro wanasheria wa takukuru Kelvin Murusuri akishilikiana na Felister Chamba wameiambia mahakama hiyo kuwa tarehe moja juni mwa mwaka 2015 Joseph  Mgile akiwa afisa mwajiri wa mgodi wa GGM aliomba  ruswa ya ngono kutoka kwa Saida Honga kwa ajiri ya kumpatia kazi.

Wanasheria hao wamendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa pamoja na Saida kuwa na vigezo vyote vya kupata kazi na kushinda kwenye kazi alizoziomba ni engineering,infrastructure,data process clack, lakini alishindwa kupata kazi kwa kigezo cha kukataa kutoa rushwa ya ngono.

Mara baada ya kumaliza kusoma shitaka hilo mshitakiwa alikana shitaka hilo na kuomba kupatiwa dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kusaini hati ya milioni saba kila mmoja.

Mshitakiwa huyo amekosa vigezo vya dhamana na kupelekwa rumande na kesi hiyo inatajiwa kuanza kusikilizwa kesho.

Imeandaliwa na Joel Maduka.


Share it:

habari

Post A Comment: