Mh,Peneza akiteta jambo na Fabiani Maenge katika eneo la Bwawa la Kasamwa. |
Muonekano wa Bwawa linalolalamikiwa na wananchi wa Kata hizo Tatu. |
Ng'ombe wakinywa maji katika Bwawa ambalo wananchi wamekuwa wakitumia maji hayo kwa mahitaji ya kila siku ya familia ikiwemo kunywa na kupikia. |
Ukaguzi wa maeneo hayo ukafanyika hapa wananchi wakimwonesha eneo hilo ambalo limeshamalizika kutengenezwa namna lilivyo kwa sasa. |
Wananchi wakielezea namna ambavyo wamekuwa wakikereka na kile ambacho kimefanyika baada ya agizo la Rais la kujenga Bwawa hilo. |
Mama akiwa amebeba ndoo akitokea kuchota maji ya Bwawa hilo. |
Wananchi wakiimba wimbo wa kutaka haki ya kupatiwa maji. |
GEITA:Wananchi
wa kata ya Kasamwa,Kanyara na Bung’wangoko Wilayani na Mkoani Geita
,wamelalamika Kutokamilika kwa Bwawa la Kasamwa na kwamba kuhusiana na pesa zilizotolewa hazijulikani
zilitumika kwa namna gani kwani hali
bado ni tete kutokana na sehemu hiyo kutumika kunyweshea mifugo.
Katika hali
isiyo ya kawaida wala ya kuridhisha madukaonilie imefika katika kata hiyo
na kukuta baadhi ya mifugo , ikiwemo Ng’ombe wakinywa maji huku akinamama wakichota maji hayo kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
Thabiza
Selemani ni mkazi wa kata ya kasamwa,ameeleza kuwa maji hayo kwa sasa ni
machafu kwani tangu Bwawa hilo kutengenezwa kutokana na agizo la Rais dk John
Pombe Magufuli hali ni mbaya limechafuka kwa kiasi kikubwa.
“Kwa namna
maji haya yalivyo kwa sasa ni bora ambayo yalikuwepo kwani yamevurugika zaidi
kwa sasa hatuwezi kufulia wala kupikia mara nyingi wanatumia watu kujengea
nyumba kiukweli tunaomba serikali isikie kilio chetu maana tunaangamia.”Alisema
Thabiza.
Almas Ngongoseke,
yeye amesema kuwa Bwawa halijajengwa bali limesafishwa kidogo tu ni kisha watu
kuwakabidhi wananchi.
Mbunge wa viti maalum jimbo la Geita(CHADEMA)
mh Upendo Peneza amefika katika bwawa hilo na kuwahaidi wananchi kufikisha
kilio chao ngazi za juu kutokana hujuma iliyofanywa ya ujenzi wa Bwawa hilo.
“Lakini
ukiliangalia hili Bwawa halifanani na kufanyiwa kazi kwa milioni 79 wananchi
walitegemea kwamba Bwawa hili lingekuwa refu kwenda chini na tope yote ingweza
kuondolewa ili wananchi wapate maji safi na salama vile vile Mh,Rais alitoa
agizo la kutenga sehemu ya kunywea mifugo na sehemu ya kuchotea maji ninawaahidi
wananchi swala hili nitalifikisha halmshauri ya mji na hata Bungeni”Alisema
Upendo.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Geita ,Mwandisi Modesti Apolinary,Amefafanua juu ya madai hayo kuwa tatizo
ni wananchi kuendelea kupeleka mifugo katika
Bwawa hilo kutoa ufafanuzi juu ya swala.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: