|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza na wananachi wa kitongoji wa mchangani kata ya Nkome. |
|
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mchangani Saimon Kinase akimweleza mkuu wa wilaya namna ambavyo watendaji wa wamekuwa wakikwamisha zoezi zima la kuwasaka wavuvi haramu |
|
Mratibu elimu kata ya Nkome Thomas Samson aliyekuwa akikaimu nafasi ya afisa mtendaji kata ,akijibu tuhuma dhidi ya kushirikiana na wavuvi haramu. |
|
Mtendaji wa kata hiyo Peter Lutangwa,akiwatuliza wananchi na kuwataka wawe makini kusikiliza mkutano. |
|
Samaki waliokamatwa. |
|
Afisa uvuvi wa kata Merina Lugumba Akijaribu kujitetea juu ya tuhuma ambazo ametuhumiwa. |
|
Mkuu wa wilaya ,Kapufi akitoa maelekezo ya kuwekwa chini ya ulinzi afisa uvuvi wa kata Merina Lugumba pamoja na mratibu elimu kata ya Nkome Thomas Samson. |
|
Wakiwa chini ya ulinzi. |
|
Wananchi wakielezea kero ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika mwalo wa Nkome. |
|
Dhana ambazo zimekuwa zikitumika katika uvuvi haramu zikiwa zimewekwa kwaajili ya kuchomwa moto. |
|
Mkuu wa Wilaya akielekea kutekeleza tendo la kuchoma moto dhana haramu za uvuvi. |
GEITA:Mkuu wa wilaya ya Wilaya Herman Kapufi ameamuru kukamatwa kwa afisa uvuvi wa kata Merina Lugumba pamoja na mratibu elimu kata ya Nkome Thomas Samson aliyekuwa akikaimu nafasi ya afisa mtendaji kata baada ya kulalamikiwa na mwenyekiti wa kitongoji cha mchangani wakiwemo na wananchi wamekuwa wakihusika kuwatetea wavuvi haramu.
Hatua hiyo imekuja baada ya siku moja kupatikana watu watano wanaodhaniwa ni wavuvi haramu kukamatwa wakiwa na matenga ya samaki wadogowadogo ambao wamevuliwa na dhana haramu huku wakikingiwa kifua na viongozi hao.
Akielezea namna ambavyo amekuwa akifanya doria ya kuwabaini wavuvi haramu Mwenyekiti wa kitongoji cha Mchangani kata ya Nkome Saimon Kinasa zoezi la kukamata wavuvi haramu limekuwa likikwamishwa na afisa uvuvi wa kata hali ambayo imesababisha kuendelea kuwepo kwa wimbi la wavuvi haramu.
“Mimi kama mwenyekiti wa kitongoji niliamua kufanya haya baada ya kutumwa na wananchi wangu walio nipigia kura walipoona samaki wengi tena wadogo wanazidi kumalizika ndani ya ziwa huku wengi wao wakitumia sumu kuwatega kwa kushirikiana na viongozi wa kata yetu”alisema Saimon.
Kutokana na tuhuma hizo Mkuu wa Wilaya Herman Kapufi aliagiza kuwekwa chini ya ulinzi kwa afisa uvuvi na mratibu wa elimu kutokana na kutokuwa upande wa Serikali nakuonekana kuendelea kuwa upande wa waranguzi ambao wamekuwa wakifanya biashara ya samaki.
“Kwa kuwa viongozi hawa wamekuwa wakishirikiana na wavuvi haramu kumaliza samaki wetu tena kwa makusudi kabisa bila kuona huruma na kutokujitambua kwamba walikuja kuwatumikia wananachi naomba wakamatwe mara moja na kuwekwa ndani” alisema Kapufi.
Madukaonline imeshuhudia askari wa TANAPA kutoka hifadhi ya Rubondo wakiendesha operesheni ya ghafla dhidi ya wavuvi wanaotumia makokoro katika ziwa victoria upande wa kitongoji cha Mchangani kata ya Nkome huku dhana haramu za kuvuliwa samaki zenye thamani ya sh. Milioni 158 zikiteketezwa kwa moto.
Imeandaliwa na Joel Maduka.
Post A Comment: