Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kimetoa wiki mbili kwa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Mkoani humo kuhakikisha inapeleka asilimia 20 katika serikali za mitaa.
Chama hicho kimeongeza kuwa ikiwa halmashauri hiyo itashindwa kutekeleza jambo hilo, kitawataka wenyeviti wa mitaa waliochaguliwa kupitia chama chao kutokufanya shughuli yeyote ya maendeleo na serikali.
Tamko hilo limetolewa jana na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Martine Moga wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Bariadi, huku akieleza madai hayo yako kisheria.
Moga alisema kuwa toka mwaka 2014 wenyeviti wa vijiji na mitaa kuchaguliwa kwao halmashauri hiyo haijapeleka asilimia 20 ya makusanyo katika serikali za mitaa, huku wenyeviti hao wakitumia pesa zao kuendesha ofisi.
Alisema uendeshaji wa ofisi kwa wenyeviti wote wa chama hicho na wengine kutoka CCM, CUF umekuwa ukitegemea pesa kutoka mfukoni mwao ambazo uzipata kwa ajili ya familia zao.
“ tunatoa muda wa siku 14 kwa uongozi wa halmshauri ya mji wa Bariadi kuhakikisha asilimia hiyo inapelekwa kwa ajili ya kuendesha ofisi na kusaidia wananchi…wakishindwa kufanya hivyo tutawataka wenyeviti kuacha kufanya kazi za serikali na maendeleo” Aliongeza
“ tunatoa muda wa siku 14 kwa uongozi wa halmshauri ya mji wa Bariadi kuhakikisha asilimia hiyo inapelekwa kwa ajili ya kuendesha ofisi na kusaidia wananchi…wakishindwa kufanya hivyo tutawataka wenyeviti kuacha kufanya kazi za serikali na maendeleo” Aliongeza
Katika hatua nyingine Katibu huyo ameitaka taasisi ya kuzua na kupamba na Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo kuingilia kati suala la utoaji dhabuni kwa wakala wa kukusanya ushuru katika mnada wa Bariadi Kidinda.
Aidha aliongeza kuwa Chama chake kimesikitishwa na hatua ya halmashauri hiyo kumwondoa katika Kamati ya fedha na mipango Diwani wao Lukonge Nyankali, na kamati hiyo kubakia madiwani kutoka chama kimoja CCM.
Post A Comment: