Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya matukio ya mauwaji yanayoendelea kutokea Mkoani hapa. |
Mtendaji wa Kata ya Bugulula Juma Choma akielezea namna walivyofanya msako wa kumsaka marehemu. |
Baadhi ya waendesha piki piki wakiwa katika hali ya majonzi kutokana na msiba wa Boda boda mwenzao. |
Mwili wa marehemu Mabula Sikitiko ukiwa umehifadhiwa katika shuka ukisubilia wataalam kwaajili ya uchunguzi. |
Wananchi wakiwa na siraha za jadi baada ya kufanya msako wa kumtafuta marehemu katika pori la nyakabale. |
Wasamaria wema wakiuwifadhi mwili huo kwaajili ya kwenda kuzikwa . |
GEITA:Mkazi
mmoja wa kijiji na kata ya Bugulula, Mabula Sikitiko mwenye umri wa miaka 18
dereva wa boda boda amekutwa ameuwawa na
watu wasio julikana katika pori lililopo mpakani mwa kijjiji cha Nyakabare na Nyawilimilwa
Wilayani Geita.
Amekutwa
akiwa ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na watu ambao bado
hawajajulikana na kisha kuibiwa pikipiki yake yenye namba za usajili MC.208 AWU.
Aidha baadhi
ya wanakijiji katika kijiji hicho,wamesema kuwa kutokea kwa tukio la namna hiyo
ni mara ya pili tangu kutokea na kwamba paka sasa bado hawajajua ni akina nani
ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya namna hiyo ambavyo ni vya kinyama.
Kamanda wa
polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo,huku akitoa wito kwa waendesha pikipiki kuwa makini na kuachana na dhana
ya kubeba watu wawili katika boda boda kwani dhana hiyo imeendelea kuwaangamiza
wengi.
Hata hivyo
kabla ya kifo hicho tarehe 22 mwezi huu majira ya saa 8:00 asubuhi marehemu
akiwa Bugulula alikokodiwa na watu wawili wasiojulikana ambapo hakurudi tena
hadi mwili wake ulipokutwa umetelekezwa porini.
Chanzo cha
mauaji hayo ni kuwania mali,jeshi la polisi linaendelea na msako ili kuwabaini
na kuwatia hatiani waliohusika na mauajihayo.
Kamanda pia
ametaja matukio mengine ya kuuwawa kwa watu katika mazingira tofauti ni pamoja
na tukio la tarehe 20 mwezi huu majira ya saa 11:30 jioni katika mgodi wa
dhahabu wa Geita uliopo kata ya mtakuja
mkazi wa mtaa wa Nyakumbu Chacha Gailigi(30) kabila mkurya ,mkulima
alifariki Dunia baada ya kudumbukia
ndani ya shimo la maji ambalo limo ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)
Tarehe 22 mwezi huu mwili wake ulionekana ukielea ndani ya maji na kuopolewa.
Kamanda
ameeleza chanzo cha tukio hilo ni kuwa Tarehe 20,mwezi huu marehemu akiwa na
Nelson Busumabu,waliingia kwa jinai mgodini hapo na walioonwa na walinzi wa
mgodi huo walianza kukimbia ili wasikamatwe na marehemu alivua viatu pamoja na
shati na kujirusha ndani ya shimo hilo la maji huku mwenzake akiendelea
kukimbia na kufanikiwa kuwatoroka walinzi hao.
Kamanda
ametoa rai kwa wananchi wanaopenda kuingia mgodini hapo kwa lengo la kutenda
uharifu kuacha mara moja ili kuepusha madhala ambayo yanaweza kuwapata.
Tukio
jingine limemuhusisha Ashura Kadoshi (50)aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye
makali kichwani na mkono wa kushoto na mtu/watu ambao bado hawajajulikana.
Imeandikwa na Joel Maduka.
Post A Comment: