Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Mh,Seleman Jafo,akitoa maagizo kwa watumishi Wilayani Mbongwe Mkoani Geita. |
GEITA:Naibu waziri wa Nchi,
Ofisi ya Raisi tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Mh,Seleman Jafo amewataka watumishi wa idara mbalimbali wilayani Mbogwe mkoani Geita
kutimiza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi kwa kuwatumikia wananchi wenye
imani kubwa na serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea mabadiliko.
Hayo ameyasema
wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe
katika ukumbi wa Casablanca,amesema watumishi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa
mazoea hali inayokwamisha utendaji kazi wa serikali na kuwataka kubadilika kwa kufanya kazi kwa
kutumia taaluma zao na kutimiza majukumu
kwa kuwatumikia wananchi.
Katika hatua nyingine
Mh,Jafo amesema wakuu wa idara mbalimbali nchini wamekuwa wakichangia kuuwa
vipaji vya watumishi kwa kushindwa kushughulikia matatizo yao kwa wakati hali
inayoshusha uwezo kwa watumishi kujituma kufanya kazi.
“Morali ya wafanyakazi
inatokana na mambo mengi jambo la kwanza ni kushughulikia madai ya watumishi, watu
maeneo mengine wanapandishana madaraja kwa upendeleo na maeneo mengine inaenda
mbali mwingine hampandishi daraja paka atoe rushwa na rushwa mbaya kuliko zote
ni rushwa ya Ngono yani mtu hampandishi mtu daraja paka amdhalilishe utu wake na
thamani yake naomba niwasihi haya mambo hatupendi yatokee Bukombe na nyinyi
wakuu wa idara fanyeni kazi kwa uwadilifu kila kitu kikae sawa”Alisema Jafo
Aidha Mh,Jaffo amewataka
wakuu wa Idara na watumishi wengine kujiamini wakati wa kazi kwa kutenda haki
kwa kila mmoja hasa katika kuwatumikia wananchi na kuacha majungu sehemu zao za kazi ili kuleta
mabadiliko na ufanisi katika kazi.
Post A Comment: