WAZAZI WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU.

Share it:
  


Kikundi cha kwaya kutoka darasa la sita shule ya Aloysius  English Medium ,wakitumbuhiza katika sherehe hizo.

Meza kuu ikifatilia kwa umakini kile kinachoendelea.

Wahitimu wa darasa la saba,wakiwa wanamsikiliza mgeni rasimi.

Wageni waalikwa pamoja na wazazi.

Wanafunzi wahitimu wakiingia uwanjani kwaajili ya burudani.'


Vijana wakionesha ustadi wao wa kuimba.

Muziki wa Dasi na wenyewe ulikuwepo.

Mkuu wa shule ,sister Zabinus Mrema akimkaribisha mgeni rasimi kugawa vyeti.

Zoezi la ugawaji wa vyeti likaendelea.





Baada ya zoezi hilo Mgeni rasimi ambae ni Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini,Constatine Kanyasu akatoa neno kwa wanafunzi.




Zoezi la kukata keki baada ya hotuba ya mgeni rasimi.





GEITA:Wazazi Na Walenzi Mkoani Geita,Wametakiwa Kuweka Nguvu Kubwa Ya Kuakikisha Wanawasomesha Watoto  Wao Na Kuachana Na Dhana Ya Kukwepa Gharama Katika Kusomesha Watoto.

Rai Hiyo Imetolewa Na Mbunge Wa Jimbo La  Geita Mjini   Constantine Kanyasu  Wakati Alipokuwa Mgeni Rasimi Katika Mahafali Ya Tatu Ya Shule Ya Msingi Ya Aloysius  English Medium Iliyopo Mkoani Hapa.

Amesema Kuwa Ni  Wajibu Wa Wazazi Kuakikisha Kwamba  Wanawajengea Mazingira Mazuri ya Watoto Kupata Elimu Bora Ambayo Itawasaidia Kukabiliana Na Swala La Utandawazi Pamoja Na Soko La Ajira.

 “Natambua Faida Ya Kusomesha Watoto Na Umuhimu Wa Elimu Napenda Kuwasihi Wazazi Wenzangu Kuweka Nguvu Kubwa Ya Kusomesha Watoto Kwani Tunaamini Kuwa Watoto Ni Taifa La Kesho.”Alisema Kanyasu.

Aidha Kwa Upande Wao Wazazi Waliokuwepo Katika Mahafali Hayo ,Samwili Hewa Na Bi Merry Peter,Wamewashauri Wazazi Kuwaendeleza Wanafunzi Waliomaliza Darasa La Saba Kwa Madarasa Ya Kidato Cha Kwanza Ya Awali Na Kuachana Na Swala La Kuwaweka Nyumbani Kusubiria Matokeo.

Hata Hivyo Wanafunzi Ambao Wamemaliza Darasa La Saba Katika Shule Hiyo, Sarafina Alex Na Aloyce Revocatus,Wamewashauri Wanafunzi Ambao Wamebaki Shuleni Hapo Kusoma Kwa Bidii  Na Kuwa Na Nidhamu Ili Waweze Kufikia Malengo Na Ndoto Walizojiwekea.

Kwaupande Wake Mwalimu Marithin Ndola,Amesema Kuwa Wamewaanda Watoto Na Kuwapa Maadili Mema Na Wanaamini Watakuwa Vizuri Na Kuwa Nandhimu Hata Baada Ya Kuwa Wamemaliza Masomo Yao Ya Darasa La Saba Shuleni Hapo.

meandaliwa Na Joel Maduka.
Share it:

habari

Post A Comment: